Tafsiri ya Ulimwegu Mpya Ayubu—Yaliyomo AYUBU YALIYOMO 1 Utimilifu wa Ayubu na mali zake (1-5) Shetani atilia shaka nia ya Ayubu (6-12) Ayubu apoteza mali na watoto wake (13-19) Ayubu hamlaumu Mungu (20-22) 2 Shetani atilia shaka tena nia ya Ayubu (1-5) Shetani aruhusiwa kugusa mwili wa Ayubu (6-8) Mke wa Ayubu: “Mtukane Mungu, ufe!” (9, 10) Ayubu atembelewa na marafiki watatu (11-13) 3 Ayubu ajuta kuzaliwa (1-26) Auliza kwa nini anateseka (20, 21) 4 Elifazi azungumza kwa mara ya kwanza (1-21) Adhihaki utimilifu wa Ayubu (7, 8) Asimulia ujumbe kutoka kwa kiumbe wa roho (12-17) ‘Mungu hana imani na watumishi wake’ (18) 5 Elifazi aendelea kuzungumza (1-27) ‘Mungu huwanasa wenye hekima katika ujanja wao’ (13) ‘Ayubu hapaswi kukataa nidhamu ya Mungu’ (17) 6 Jibu la Ayubu (1-30) Adai kwamba ana sababu ya kulia (2-6) Wafariji wake ni wenye hila (15-18) “Maneno ya unyoofu hayaumizi!” (25) 7 Ayubu aendelea kujibu (1-21) Maisha ni kama kazi ya kulazimishwa (1, 2) “Kwa nini umenifanya niwe shabaha yako?” (20) 8 Bildadi azungumza kwa mara ya kwanza (1-22) Adai kwamba watoto wa Ayubu wametenda dhambi (4) ‘Ikiwa ungekuwa safi, Mungu angekulinda’ (6) Adai kwamba Ayubu amemkataa Mungu (13) 9 Jibu la Ayubu (1-35) Mwanadamu anayeweza kufa hawezi kushindana na Mungu (2-4) ‘Mungu hufanya mambo yasiyochunguzika’ (10) Mtu hawezi kubishana na Mungu (32) 10 Ayubu aendelea kujibu (1-22) ‘Kwa nini Mungu anapambana nami?’ (2) Mungu si kama Ayubu anayeweza kufa (4-12) ‘Naomba nipate kitulizo kidogo’ (20) 11 Sofari azungumza kwa mara ya kwanza (1-20) Amshutumu Ayubu kwa sababu ya maneno yake yasiyo na maana (2, 3) Amwambia Ayubu aache uovu (14) 12 Jibu la Ayubu (1-25) “Mimi si duni kwenu” (3) “Nimekuwa kichekesho” (4) ‘Mungu ana hekima’ (13) Mungu ni mkuu kuliko waamuzi na wafalme (17, 18) 13 Ayubu aendelea kujibu (1-28) ‘Ni afadhali nizungumze na Mungu’ (3) ‘Ninyi ni matabibu wasiofaa kitu’ (4) “Najua sina kosa” (18) Auliza kwa nini Mungu anamwona kuwa adui (24) 14 Ayubu aendelea kujibu (1-22) Maisha ya mwanadamu ni mafupi na yamejaa taabu (1) “Hata mti una tumaini” (7) “Laiti ungenificha Kaburini!” (13) “Mtu akifa, je, anaweza kuishi tena?” (14) Mungu ataitamani sana kazi ya mikono yake (15) 15 Elifazi azungumza kwa mara ya pili (1-35) Adai kwamba Ayubu hamwogopi Mungu (4) Asema Ayubu ana kimbelembele (7-9) ‘Mungu hana imani na watakatifu wake’ (15) ‘Anayeteseka ni mwovu’ (20-24) 16 Jibu la Ayubu (1-22) ‘Ninyi ni wafariji wasumbufu!’ (2) Adai kwamba Mungu anamfanya kuwa shabaha yake (12) 17 Ayubu aendelea kujibu (1-16) “Wadhihaki wananizunguka” (2) “Amenifanya niwe kitu cha kudharauliwa” (6) “Kaburi litakuwa makao yangu” (13) 18 Bildadi azungumza kwa mara ya pili (1-21) Aeleza yatakayowapata waovu (5-20) Adai Ayubu hamjui Mungu (21) 19 Jibu la Ayubu (1-29) Akataa kukemewa na “rafiki” zake (1-6) Asema kwamba ameachwa (13-19) “Mkombozi wangu yuko hai” (25) 20 Sofari azungumza kwa mara ya pili (1-29) Adai kwamba Ayubu amemtukana (2, 3) Adai kwamba Ayubu ni mwovu (5) Adai kwamba Ayubu anafurahia dhambi (12, 13) 21 Ayubu ajibu (1-34) ‘Kwa nini waovu wanafanikiwa?’ (7-13) Afichua hila za “wafariji” wake (27-34) 22 Elifazi azungumza kwa mara ya tatu (1-30) ‘Mwanadamu ana faida gani kwa Mungu?’ (2, 3) Adai kwamba Ayubu ni mwenye pupa na hatendi haki (9) ‘Mrudie Mungu, utarudishiwa hali njema’ (23) 23 Ayubu ajibu (1-17) Ataka kupeleka kesi yake mbele za Mungu (1-7) Asema kwamba hampati Mungu (8, 9) “Nimefuata njia yake bila kukengeuka” (11) 24 Ayubu aendelea kujibu (1-25) ‘Kwa nini Mungu haweki wakati wa hukumu?’ (1) Asema kwamba Mungu ameruhusu uovu (12) Watenda dhambi wanapenda giza (13-17) 25 Bildadi azungumza kwa mara ya tatu (1-6) ‘Mwanadamu anawezaje kuwa bila hatia mbele za Mungu?’ (4) Adai kwamba utimilifu wa mwanadamu ni wa bure (5, 6) 26 Ayubu ajibu (1-14) “Jinsi mlivyomsaidia mtu asiye na uwezo!” (1-4) ‘Mungu anaining’iniza dunia mahali pasipo na kitu’ (7) ‘Ni kingo tu za njia za Mungu’ (14) 27 Ayubu aazimia kuendelea kuwa mtimilifu (1-23) “Sitaukana utimilifu wangu” (5) Anayemkataa Mungu hana tumaini (8) “Kwa nini mazungumzo yenu hayana maana yoyote?” (12) Mtu mwovu habaki na chochote (13-23) 28 Ayubu aonyesha tofauti iliyopo kati ya hazina za dunia na hekima (1-28) Jitihada za wanadamu za kuchimba madini (1-11) Hekima ina thamani kuliko lulu (18) Kumwogopa Yehova ndiyo hekima ya kweli (28) 29 Ayubu akumbuka maisha mazuri aliyokuwa nayo kabla ya mateso (1-25) Aliheshimiwa kwenye lango la jiji (7-10) Jinsi alivyokuwa akitenda haki awali (11-17) Kila mtu alisikiliza ushauri wake (21-23) 30 Ayubu aeleza jinsi maisha yake yalivyobadilika (1-31) Adhihakiwa na watu wasiofaa kitu (1-15) Yaonekana ni kama Mungu hamsaidii (20, 21) “Ngozi yangu imekuwa nyeusi” (30) 31 Ayubu atetea utimilifu wake (1-40) “Agano na macho yangu” (1) Aomba Mungu ampime (6) Hakuwa mzinzi (9-12) Hakupenda pesa (24, 25) Hakuabudu sanamu (26-28) 32 Kijana Elihu ajiunga na mazungumzo (1-22) Amkasirikia Ayubu na rafiki zake (2, 3) Alisubiri kwa heshima kabla ya kuzungumza (6, 7) Umri peke yake haumfanyi mtu awe na hekima (9) Elihu atamani kuongea (18-20) 33 Elihu amkaripia Ayubu kwa sababu ya kujiona kuwa mwadilifu (1-33) Fidia yapatikana (24) Kurudia nguvu za ujana (25) 34 Elihu atetea haki ya Mungu na njia zake (1-37) Ayubu asema kwamba Mungu alimnyima haki (5) Mungu wa kweli hawezi kamwe kutenda uovu (10) Ayubu hana ujuzi (35) 35 Elihu ataja mawazo yasiyofaa ya Ayubu (1-16) Ayubu asema yeye ni mwadilifu kuliko Mungu (2) Mungu yuko juu sana, haathiriwi na dhambi (5, 6) Ayubu anapaswa kumngojea Mungu (14) 36 Elihu autukuza ukuu wa Mungu usiochunguzika (1-33) Wanaotii wanafanikiwa; wanaomkataa Mungu wanakataliwa (11-13) ‘Ni nani aliye mfundishaji kama Mungu?’ (22) Ayubu anapaswa kumtukuza Mungu (24) “Mungu ni mkuu kuliko tunavyoweza kujua” (26) Mungu hudhibiti mvua na radi (27-33) 37 Nguvu za asili zinafunua ukuu wa Mungu (1-24) Mungu anaweza kusimamisha shughuli za wanadamu (7) ‘Tafakari kazi za Mungu zinazostaajabisha’ (14) Wanadamu hawawezi kumwelewa Mungu (23) Hakuna mwanadamu anayepaswa kufikiri kwamba ana hekima (24) 38 Yehova afundisha kuhusu udogo wa mwanadamu (1-41) ‘Ulikuwa wapi nilipoiumba dunia?’ (4-6) Wana wa Mungu walishangilia kwa sauti (7) Maswali kuhusu matukio ya asili (8-32) “Sheria zinazoongoza mbingu” (33) 39 Uumbaji wa wanyama waonyesha ujinga wa mwanadamu (1-30) Mbuzi wa milimani na paa (1-4) Punda mwitu (5-8) Fahali mwitu (9-12) Mbuni (13-18) Farasi (19-25) Kipanga na tai (26-30) 40 Yehova amuuliza maswali zaidi (1-24) Ayubu akiri hana la kusema (3-5) “Je, utatilia shaka haki yangu?” (8) Mungu aeleza kuhusu nguvu za Behemothi (15-24) 41 Mungu aeleza kuhusu Lewiathani anayestaajabisha (1-34) 42 Ayubu amjibu Yehova (1-6) Rafiki watatu wa Ayubu washutumiwa (7-9) Yehova ambariki tena Ayubu (10-17) Wana na mabinti wa Ayubu (13-15)