Tafsiri ya Ulimwegu Mpya Kumbukumbu la Torati—Yaliyomo KUMBUKUMBU LA TORATI YALIYOMO 1 Kuondoka Mlima Horebu (1-8) Wakuu na waamuzi wawekwa (9-18) Watu wakosa kutii kule Kadesh-barnea (19-46) Waisraeli wakataa kuingia katika ile nchi (26-33) Washindwa kuteka Kanaani (41-46) 2 Kutangatanga nyikani kwa miaka 38 (1-23) Wamshinda Mfalme Sihoni wa Heshboni (24-37) 3 Wamshinda Mfalme Ogu wa Bashani (1-7) Kugawanywa kwa nchi upande wa mashariki wa Yordani (8-20) Yoshua aambiwa asiogope (21, 22) Musa hataingia katika nchi hiyo (23-29) 4 Waagizwa watii (1-14) Msisahau matendo ya Mungu (9) Yehova anataka aabudiwe yeye peke yake (15-31) Hakuna Mungu mwingine ila Yehova (32-40) Majiji ya makimbilio upande wa mashariki wa Yordani (41-43) Wapewa Sheria (44-49) 5 Agano la Yehova kule Horebu (1-5) Amri Kumi zarudiwa (6-22) Watu waogopa kwenye Mlima Sinai (23-33) 6 Mpende Yehova kwa moyo wako wote (1-9) “Sikilizeni, enyi Waisraeli” (4) Wazazi wanapaswa kuwafundisha watoto (6, 7) Msimsahau Yehova (10-15) Msimjaribu Yehova (16-19) Kiambieni kizazi kinachofuata (20-25) 7 Mataifa saba yataangamizwa (1-6) Sababu ya Waisraeli kuchaguliwa (7-11) Utii utawaletea mafanikio wakati ujao (12-26) 8 Baraka kutoka kwa Yehova zatajwa tena (1-9) “Haishi kwa mkate tu” (3) Msimsahau Yehova (10-20) 9 Sababu ya Waisraeli kupewa ile nchi (1-6) Waisraeli wamkasirisha Yehova mara nne (7-29) Ndama wa dhahabu (7-14) Musa aingilia kati (15-21, 25-29) Wamkasirisha mara tatu zaidi (22) 10 Mabamba mawili yatengenezwa tena (1-11) Analotaka Yehova (12-22) Mwogopeni na kumpenda Yehova (12) 11 Mmeuona ukuu wa Yehova (1-7) Nchi Iliyoahidiwa (8-12) Thawabu za kutii (13-17) Maneno ya Mungu yakaziwe katika mioyo (18-25) “Baraka na laana” (26-32) 12 Abuduni mahali ambapo Mungu amechagua (1-14) Waruhusiwa kula nyama lakini si damu (15-28) Msinaswe na miungu mingine (29-32) 13 Jinsi ya kuwatendea waasi imani (1-18) 14 Njia zisizofaa za kuomboleza (1, 2) Vyakula safi na visivyo safi (3-21) Sehemu ya kumi kwa ajili ya Yehova (22-29) 15 Madeni yafutwa kila mwaka wa saba (1-6) Kuwasaidia maskini (7-11) Kuwaachilia huru watumwa kila mwaka wa saba (12-18) Kutoboa sikio la mtumwa kwa msumari (16, 17) Wazaliwa wa kwanza wa wanyama watakaswa (19-23) 16 Pasaka; Sherehe ya Mikate Isiyo na Chachu (1-8) Sherehe ya Majuma (9-12) Sherehe ya Vibanda (13-17) Kuwaweka waamuzi (18-20) Vitu vya ibada vilivyokatazwa (21, 22) 17 Dhabihu zisiwe na kasoro (1) Kushughulikia uasi imani (2-7) Kuamua kesi ngumu (8-13) Maagizo kwa ajili ya mfalme atakayetawala (14-20) Mfalme aandike nakala ya Sheria (18) 18 Fungu la makuhani na Walawi (1-8) Mazoea ya kuwasiliana na roho waovu yakatazwa (9-14) Nabii kama Musa (15-19) Jinsi ya kuwatambua manabii wa uwongo (20-22) 19 Hatia ya damu na majiji ya makimbilio (1-13) Alama za mipaka zisisogezwe (14) Mashahidi mahakamani (15-21) Mashahidi wawili au watatu wahitajika (15) 20 Sheria za vita (1-20) Wale ambao hawakuruhusiwa kwenda vitani (5-9) 21 Mauaji yaliyofanywa na watu wasiojulikana (1-9) Kuoa wanawake mateka (10-14) Haki ya mzaliwa wa kwanza (15-17) Mwana mkaidi (18-21) Mtu aliyetundikwa mtini amelaaniwa (22, 23) 22 Kuheshimu wanyama wa jirani (1-4) Kuvaa nguo za watu wa jinsia tofauti (5) Kuwatendea wanyama kwa fadhili (6, 7) Ukuta unaozunguka ukingo wa paa (8) Michanganyiko isiyofaa (9-11) Vishada vya nguo (12) Sheria kuhusu kukiuka maadili ya ngono (13-30) 23 Wasioruhusiwa katika kutaniko la Mungu (1-8) Usafi wa kambi (9-14) Watumwa waliokimbia (15, 16) Ukahaba wakatazwa (17, 18) Riba na nadhiri (19-23) Vitu ambavyo wapita njia wanaruhusiwa kula (24, 25) 24 Ndoa na talaka (1-5) Kuheshimu uhai (6-9) Kuwajali maskini (10-18) Sheria kuhusu kuokota masalio (19-22) 25 Sheria kuhusu kumpiga mtu viboko (1-3) Usimfunge kinywa ng’ombe dume anapopura (4) Ndoa ya ndugu mkwe (5-10) Kumkamata mtu sehemu zisizofaa anapopigana (11, 12) Mizani na vipimo sahihi (13-16) Waamaleki wataangamizwa (17-19) 26 Kutoa mavuno ya kwanza (1-11) Sehemu ya kumi iliyotolewa mara ya pili (12-15) Waisraeli ni mali ya pekee ya Yehova (16-19) 27 Sheria itaandikwa kwenye mawe (1-10) Kwenye Mlima Ebali na Mlima Gerizimu (11-14) Laana zatangazwa (15-26) 28 Baraka za kutii (1-14) Laana za kutotii (15-68) 29 Agano pamoja na Waisraeli kule Moabu (1-13) Onyo kuhusu kutotii (14-29) Mambo yaliyofichwa, mambo yaliyofunuliwa (29) 30 Kumrudia Yehova (1-10) Amri za Yehova si ngumu sana (11-14) Kuchagua kati ya uzima na kifo (15-20) 31 Musa akaribia kufa (1-8) Sheria yasomwa hadharani (9-13) Yoshua awekwa kuwa kiongozi (14, 15) Uasi wa Waisraeli watabiriwa (16-30) Wimbo wa kuwafundisha Waisraeli (19, 22, 30) 32 Wimbo wa Musa (1-47) Yehova ni Mwamba (4) Waisraeli wamsahau Mwamba wao (18) “Kisasi ni changu” (35) “Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake” (43) Musa atafia juu ya Mlima Nebo (48-52) 33 Musa ayabariki makabila (1-29) ‘Mikono ya milele’ ya Yehova (27) 34 Yehova amwonyesha Musa ile nchi (1-4) Kifo cha Musa (5-12)