WIMBO NA. 162
Uhitaji Wangu wa Kiroho
1. Mungu alituumba
Tukiwa na tamaa:
Yenye nguvu ya kujua,
Lengo la kuishi.
Wengi hutamauka,
Neno lake ladumu—
Linatupa tumaini,
Na shangwe ya kweli.
(KORASI)
Mimi nitamsifu,
Mungu wangu sikuzote.
N’tampa maisha yangu,
Naye ataanda’.
Nitajilisha
Kiroho kweli.
2. Natafuta wakati
Kujilisha kiroho,
Hunifanya, niwe huru
Hunisaidia.
Wengi wanapuuza,
Nasali wakubali.
Na wapate utulivu,
Shangwe kama yangu.
(KORASI)
Mimi nitamsifu,
Mungu wangu sikuzote.
N’tampa maisha yangu,
Naye ataanda’.
Nitajilisha
Kiroho kweli.
Mimi nitamsifu,
Mungu wangu sikuzote.
N’tampa maisha yangu,
Naye ataanda’.
Nitajilisha
Kiroho kweli.
Mimi nitamsifu,
Mungu wangu sikuzote.
N’tampa maisha yangu,
Naye ataanda’.
Nitajilisha
Kiroho kweli.
(Ona pia Zab. 1:1, 2; 112:1; 119:97; Isa. 40:8; Mt. 5:6; 16:24; 2 Tim. 4:4.)