Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb 102
  • Ufunuo kwa Yohana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ufunuo kwa Yohana
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb 102
Mtume Yohana akiandika kitabu cha Ufunuo

SOMO LA 102

Ufunuo kwa Yohana

Mtume Yohana alipokuwa mfungwa katika kisiwa cha Patmo, Yesu alimwonyesha mfuatano wa maono 16, au picha, kuhusu wakati ujao. Maono hayo yalionyesha jinsi jina la Yehova litakavyotakaswa, jinsi Ufalme wake utakavyokuja, na jinsi mapenzi yake yatakavyotendeka hapa duniani kama ilivyo mbinguni.

Katika mojawapo ya maono hayo, Yohana anamwona Yehova akiwa katika kiti chake cha ufalme mbinguni, naye alikuwa amezungukwa na wazee 24 waliovikwa mavazi meupe na juu ya vichwa vyao kulikuwa na mataji ya dhahabu. Mwanga wa umeme na sauti za ngurumo zinatoka katika kile kiti cha ufalme. Wale wazee 24 wanainama mbele za Yehova na kumwabudu. Katika maono mengine, Yohana anaona umati mkubwa kutoka kwa mataifa, vikundi vya watu, na lugha zote ukimwabudu Yehova. Mwana-Kondoo, ambaye ni Yesu, anawachunga na kuwaongoza kwenye maji ya uzima. Baadaye, katika maono mengine, Yesu anaanza kutawala akiwa Mfalme mbinguni, pamoja na wale wazee 24. Katika maono yanayofuata, Yohana anamwona Yesu akipigana na yule joka mkubwa, ambaye ni Shetani, na roho wake waovu. Yesu akawatupa kutoka mbinguni hadi chini duniani.

Jesus and the 144,000 on Mount Zion

Kisha Yohana akaona maono yenye kupendeza ya Mwana-Kondoo na wale 144,000 wakiwa wamesimama juu ya Mlima Sayuni. Pia, akamwona malaika akiruka kotekote duniani na kuwaambia watu wamwogope Mungu na kumpa utukufu.

Katika maono yanayofuata, vita vya Har–Magedoni vinapiganwa. Katika vita hivyo, Yesu na majeshi yake wanaushinda mfumo mwovu wa Shetani. Katika maono ya mwisho, Yohana anaona kwamba mbinguni na duniani kuna upatano kamili. Shetani na uzao wake wanaangamizwa kabisa. Wote walio mbinguni na duniani wanalitukuza jina la Yehova na kumwabudu yeye peke yake.

“Nami nitaweka uadui kati yako na mwanamke na kati ya uzao wako na uzao wake. Yeye atakuponda kichwa, nawe utamuuma kisigino.”​—Mwanzo 3:15

Maswali: Yohana aliona maono mangapi? Yesu atafanya nini wakati wa vita vya Har–Magedoni?

Ufunuo 1:1-3; 4:1-11; 7:4, 9-17; 11:15-18; 12:5-12; 14:6, 7; 16:14, 16; 21:5

    Tanzanian sign language publications (2020-2026)
    Toka
    Ingia
    • Lugha ya Alama ya Tanzania
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki