WIMBO NA. 81
Maisha ya Painia
- 1. Jua lachomoza, kunapambazuka. - Macho ni mazito, - Twasali kisha twaondoka - Tabasamu nyingi, wanasikiliza. - Hata wasiposikiliza, - Hatuchoki kamwe. - (KORASI) - Ni maisha yetu; - Tumeyachagua. - Kufanya mapenzi ya Mungu - Tutavumilia, - Kuwe mvua, jua. - Kwa kuwa twampenda sana Yehova. 
- 2. Mwishoni mwa siku, jua linatua. - Japo tumechoka - Moyoni tunayo furaha. - Ni maisha yetu, ya kujidhabihu. - Yehova twashukuru, - Kwa baraka zako nyingi. - (KORASI) - Ni maisha yetu; - Tumeyachagua. - Kufanya mapenzi ya Mungu - Tutavumilia, - Kuwe mvua, jua. - Kwa kuwa twampenda sana Yehova. 
(Ona pia Yos. 24:15; Zab. 92:2; Rom. 14:8.)