WIMBO NA. 135
Mwaliko Wenye Upendo wa Yehova: “Uwe na Hekima, Mwanangu”
- 1. Binti na mwanangu, - nipe moyo wako. - Apate kuona - yule mdhihaki. - Nawe unitumikie - kwa kupenda; - Na ulimwengu - uone wanipenda. - (KORASI) - Binti yangu, nawe mwanangu, - Furahisha moyo wangu. - Nitumikie kwa hiari, - Na kusifu jina langu. 
- 2. Nitumikie kwa - shangwe na furaha. - Ujapoanguka, - Nitakuinua. - Hata ukivunjwa moyo - na yeyote, - Kumbuka ninakupenda - sikuzote. - (KORASI) - Binti yangu, nawe mwanangu, - Furahisha moyo wangu. - Nitumikie kwa hiari, - Na kusifu jina langu. 
(Ona pia Kum. 6:5; Mhu. 11:9; Isa. 41:13.)