Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ezekieli 19
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Ezekieli—Yaliyomo

      • Wimbo wa huzuni kwa ajili ya wakuu wa Israeli (1-14)

Ezekieli 19:1

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “wimbo wa maombolezo.”

Ezekieli 19:2

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “wanasimba wenye manyoya marefu shingoni.”

Ezekieli 19:3

Marejeo

  • +2Nya 36:1

Ezekieli 19:4

Marejeo

  • +2Fa 23:31-34; 2Nya 36:4; Yer 22:11, 12

Ezekieli 19:6

Marejeo

  • +Yer 22:17

Ezekieli 19:7

Marejeo

  • +Met 28:15

Ezekieli 19:10

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “kama mzabibu katika shamba lako la mizabibu.”

Marejeo

  • +Zb 80:8; Isa 5:7

Ezekieli 19:11

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “fimbo zenye nguvu.”

Ezekieli 19:12

Marejeo

  • +Isa 5:5; Eze 15:6
  • +2Fa 23:34; 24:6; 25:5-7
  • +Kum 32:22; Eze 15:4

Ezekieli 19:13

Marejeo

  • +Kum 28:48; Yer 17:5, 6; 52:27

Ezekieli 19:14

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “fimbo zake.”

Marejeo

  • +Eze 17:16, 18

Jumla

Eze. 19:32Nya 36:1
Eze. 19:42Fa 23:31-34; 2Nya 36:4; Yer 22:11, 12
Eze. 19:6Yer 22:17
Eze. 19:7Met 28:15
Eze. 19:10Zb 80:8; Isa 5:7
Eze. 19:12Isa 5:5; Eze 15:6
Eze. 19:122Fa 23:34; 24:6; 25:5-7
Eze. 19:12Kum 32:22; Eze 15:4
Eze. 19:13Kum 28:48; Yer 17:5, 6; 52:27
Eze. 19:14Eze 17:16, 18
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Ezekieli 19:1-14

Ezekieli

19 “Nawe lazima uimbe wimbo wa huzuni* kuhusu wakuu wa Israeli, 2 useme,

‘Mama yako alikuwa nani? Simba jike kati ya simba.

Alilala kati ya wanasimba wenye nguvu* naye akawalea watoto wake.

 3 Alimlea mmoja wa watoto wake, akawa mwanasimba mwenye nguvu.+

Naye akajifunza jinsi ya kurarua mawindo,

Akamnyafua hata mwanadamu.

 4 Mataifa yalisikia kumhusu na wakamkamata katika shimo lao,

Nao wakamleta kwa kulabu nchini Misri.+

 5 Mama huyo alisubiri na hatimaye akaona hakuna tumaini kwamba atarudi.

Basi akamchukua mwingine kati ya watoto wake na kumtuma akiwa mwanasimba mwenye nguvu.

 6 Yeye pia alitembea huku na huku kati ya simba, naye akawa mwanasimba mwenye nguvu.

Akajifunza jinsi ya kurarua mawindo, na hata akawanyafua wanadamu.+

 7 Akazungukazunguka katika minara yao yenye ngome na kuyaharibu majiji yao,

Hivi kwamba nchi iliyo ukiwa ikajaa sauti ya mngurumo wake.+

 8 Mataifa ya wilaya jirani yalikuja dhidi yake ili kuutandaza wavu wao juu yake,

Naye akanaswa katika shimo lao.

 9 Wakamweka katika kizimba kwa kulabu na kumpeleka kwa mfalme wa Babiloni.

Wakamfunga huko ili sauti yake isisikike tena kwenye milima ya Israeli.

10 Mama yako alikuwa kama mzabibu+ katika damu yako,* uliopandwa kando ya maji.

Ukazaa matunda na kujaa matawi kwa sababu ya maji mengi.

11 Nao ukatokeza matawi yenye nguvu,* yanayofaa kuwa fimbo za ufalme za watawala.

Ukakua, ukawa mrefu kuliko miti mingine,

Nao ukaonekana kwa sababu ya urefu wake na wingi wa majani yake.

12 Lakini aling’olewa kwa ghadhabu+ na kutupwa chini ardhini,

Na upepo wa mashariki ukayakausha matunda yake.

Matawi yake yenye nguvu yalikatwa yakakauka,+ na moto ukayateketeza.+

13 Sasa amepandwa nyikani,

Katika nchi isiyo na maji na yenye kiu.+

14 Moto ukaenea kutoka kwenye matawi yake* na kuteketeza machipukizi yake na matunda yake,

Na hakuna tawi lenye nguvu lililobaki, hakuna fimbo ya mfalme ya kutawala.+

“‘Huo ni wimbo wa huzuni, nao utatumiwa kama wimbo wa huzuni.’”

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki