WIMBO NA. 73
Tupe Ujasiri
- 1. Tutangazapo Ufalme, - Na kukushuhudia. - Kuna wapinzani wengi, - Wanaotudhihaki. - Hatutawaogopa, - Kwa kuwa tunakutii. - Tupe roho yako twaomba, - Ee Yehova twakusihi. - (KORASI) - Tupe ujasiri Baba; - Tushinde woga wetu. - Tupe uhakika Baba, - Tuzidi kuhubiri. - Siku ya Har-Magedoni, - Twajua iko karibu, - Tupe ujasiri Baba. - Twakuomba. 
- 2. Japo twaweza kuhofu, - Wajua umbo letu. - Waahidi kutulinda, - Na kututegemeza. - Wanaotunyanyasa, - Wazidipo kututisha, - Tuwezeshe kusonga mbele, - Kutangaza jina lako. - (KORASI) - Tupe ujasiri Baba; - Tushinde woga wetu. - Tupe uhakika Baba, - Tuzidi kuhubiri. - Siku ya Har-Magedoni, - Twajua iko karibu, - Tupe ujasiri Baba. - Twakuomba. 
(Ona pia 1 The. 2:2; Ebr. 10:35.)