WIMBO NA. 126
Uwe Macho, Simama Imara, Uwe na Nguvu
- 1. Uwe macho na imara, - Azimia kudumu. - Tenda kama mwanamume, - Ushinde majaribu. - Kristo Yesu msikilize, - Usimame upande wake. - (KORASI) - Uwe macho na mwenye nguvu! - Udumu hadi mwisho. 
- 2. Uwe macho na kukesha, - Na tayari kutii. - Tii mwongozo wa Kristo, - Kupitia mtumwa. - Tii shauri la wazee, - Walindao kondoo zake. - (KORASI) - Uwe macho na mwenye nguvu! - Udumu hadi mwisho. 
- 3. Uwe macho kutetea, - Ukweli kwa bidii. - Japo adui ni wengi, - Hubiri hadi mwisho. - Shiriki kumsifu Mungu. - Siku Yake iko karibu. - (KORASI) - Uwe macho na mwenye nguvu! - Udumu hadi mwisho. 
(Ona pia Mt. 24:13; Ebr. 13:7, 17; 1 Pet. 5:8.)