WIMBO NA. 61
Songeni Mbele, Enyi Mashahidi!
- 1. Watu wa Mungu wameazimia, - Kazi ya kuhubiri itatimia. - Shetani akiwavamia, - Kwa nguvu za Mungu wavumilia. - (KORASI) - Haya tusonge mbele Ee Mashahidi! - Kufanya kazi ya Mungu na tuzidi! - Yaja Paradiso aliyoahidi, - Yehova Mungu tumhimidi. 
- 2. Askari wa Yehova wanakesha. - Ulimwengu hautawatetemesha. - Na uovu wajiepusha. - Utimilifu wetu twadumisha. - (KORASI) - Haya tusonge mbele Ee Mashahidi! - Kufanya kazi ya Mungu na tuzidi! - Yaja Paradiso aliyoahidi, - Yehova Mungu tumhimidi. 
- 3. Enzi ya Mungu yadharauliwa. - Jina lake kuu limechafuliwa. - Karibuni litatakaswa. - Mbele za wote litatambulishwa. - (KORASI) - Haya tusonge mbele Ee Mashahidi! - Kufanya kazi ya Mungu na tuzidi! - Yaja Paradiso aliyoahidi, - Yehova Mungu tumhimidi. 
(Ona pia Kut. 9:16; Flp. 1:7; 2 Tim. 2:3, 4; Yak. 1:27.)