WIMBO NA. 120
Igeni Upole wa Kristo
- 1. Bwana Yesu hakuwa na kiburi; - Hakujitakia makuu kamwe. - Alikuwa na jukumu muhimu; - Lakini kajishusha sikuzote. 
- 2. Nyote mlio na mahangaiko, - Ichukueni nira yake Kristo. - Mtapata burudisho la nafsi; - Bwana wetu ana tabia-pole. 
- 3. ‘Nyote ni ndugu,’ kasema Bwanetu. - Msiwe mkitafuta makuu. - Wapole wana thamani kwa Mungu; - Watairithi dunia milele. 
(Ona pia Met. 3:34; Mt. 5:5; 23:8; Rom. 12:16.)