WIMBO NA. 100
Wakaribisheni
- 1. Yehova huonyesha ukarimu. - Ubaguzi hana, si mdhalimu - Jua nayo mvua, - hanyimi yeyote. - Hutoa chakula kwa wote. - Tuwafadhilipo watu wa chini, - Twamwiga Yehova, Anathamini. - Naye Baba yetu, - atatufadhili, - Kwa wema wetu na fadhili. 
- 2. Hatuwezi kujua matokeo, - Ya kutokuwa na upendeleo. - Hata iwe kwamba, - hatuwafahamu, - Twawakaribisha kwa hamu. - Nasi twawaambia, ‘karibuni! ’ - Wajistareheshe bila huzuni. - Mungu awajua - wote wamwigao. - Wawafadhilio wenzao. 
(Ona pia Mdo. 16:14, 15; Rom. 12:13; 1 Tim. 3:2; Ebr. 13:2; 1 Pet. 4:9.)