WIMBO NA. 33
Mtupie Yehova Mzigo Wako
- 1. Ee Yehova nakuomba, - Usijifiche mbali. - Sikiliza, unijibu, - Ili nisiogope. - (KORASI) - Mtupie Yah mzigo; - Naye atakutegemeza. - Hataacha utikiswe, - Atakuimarisha. 
- 2. Kama ningekuwa njiwa, - Ningeruka nyikani, - Mbali na watu waovu, - Watendao jeuri. - (KORASI) - Mtupie Yah mzigo; - Naye atakutegemeza. - Hataacha utikiswe, - Atakuimarisha. 
- 3. Yehova hutufariji, - Na kutupa amani. - Ijapo tunalemewa, - Ana fadhili nyingi. - (KORASI) - Mtupie Yah mzigo; - Naye atakutegemeza. - Hataacha utikiswe, - Atakuimarisha. 
(Ona pia Zab. 22:5; 31:1-24.)