Kujikumbusha Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
Maulizo yafuatayo yatajibiwa kwa maneno tu kwenye Shule ya Huduma ya Kitheokrasi mnamo juma toka Februari 24, 2003. Kwa dakika 30, mwangalizi wa shule ataongoza kujikumbusha kwenye kutegemea habari iliyozungumziwa katika migawo ya majuma ya Januari 6 mpaka Februari 24, 2003. [Taarifa: Mahali ambapo hakuna kichapo kinachoonyeshwa baada ya ulizo, utahitaji kufanya utafiti wako mwenyewe ili kupata majibu.—Ona kitabu Shule ya Huduma, uku. 36-7.]
SIFA ZA USEMI
1. Kweli au Si Kweli: Ufunguo wa kusoma kwa usahihi ni kuhakikisha kwamba yale yanayosomwa yanaonekana kuwa sawa, hata ikiwa yanatofautiana kidogo na yale yanayoandikwa. Eleza. [be-SW uku. 83]
2. Jaza Nafasi Zilizo Wazi: Ili kusoma kwa usahihi, mtu anapaswa _________________________ na kusoma kwa sauti. [be-SW uku. 85]
3. Kwa nini ni jambo la maana kusema kwa njia inayoeleweka wazi? (1 Kor. 14:8, 9) [be-SW uku. 86]
4. Ni mambo gani yanayoweza kufanya usemi usiwe wazi, na tunaweza kufanya nini ili kusema kwa njia inayoeleweka waziwazi zaidi? [be-SW uku. 87-8]
5. Ni maneno gani unayofikiri unahitaji kujizoeza kutamka vizuri kati ya yale yaliyotumiwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi mnamo miezi miwili iliyotangulia? [be-SW uku. 92]
MGAWO NA. 1
6. Kweli au Si Kweli: Macho yetu yanaweza kutusaidia kusikiliza. Eleza. [be-SW uku. 14]
7. Jaza Nafasi Zilizo Wazi: _________________________, _________________________, na _________________________ vyote vinatumika kama viishara vya wakati vilivyotolewa na Mungu. [si-SW uku. 279 fu. 7]
8. Jaza Nafasi Zilizo Wazi: Katika matumizi ya Biblia, neno “siku” linaweza kurejezea kipindi cha saa _________________________, saa _________________________, miaka _________________________ au _________________________; muktadha ndio unaoonyesha maana ambayo katika hiyo neno hilo linatumiwa [si-SW uku. 279 fu. 8]
9. Mifano ya Hana, Marko, na Eliya inatusaidiaje kupambana na kivunja-moyo kwa mafanikio? Tunawezaje kutumia mifano hiyo ili kusaidia wengine? [w01-SW 2/1 uku. 20-3]
10. Kuelewa michezo ya zamani ya riadha kunatoaje mwangaza kuhusu maandiko fulani ya Biblia? Habari hiyo inapaswa kuwa na uvutano gani juu ya maisha zetu? [w01-SW 1/1 uku. 28-31]
USOMAJI WA BIBLIA WA KILA JUMA
11. Kweli au Si Kweli: Kwa kuwa Ufalme wa Mungu ulisimamishwa mbinguni mnamo mwaka wa 1914, haifai tena kuomba, “Acha ufalme wako uje.” (Mt. 6:10) Eleza. [be-SW uku. 279; w96-SW 6/1 uku. 31]
12. Kweli au Si Kweli: Maneno ya Yesu yanayopatikana kwenye Mathayo 11:24 yanamaanisha kwamba wale ambao Yehova aliharibu kwa moto katika Sodoma na Gomora watafufuliwa. Eleza.
13. Chagua Jibu Sahihi: Mtumwa mwaminifu na mwenye busara anayetajwa na Yesu kwenye Mathayo 24:45-47 ni (a) Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova; (b) Wakristo wote wapakwa-mafuta wakiwa kikundi duniani wakati wowote; (c) Yesu Kristo mwenyewe. Mtumwa huyo anatoa chakula cha kiroho kwa wakati unaofaa kwa ‘watumishi wa nyumbani,’ ambao wanawakilisha (a) wapakwa-mafuta wakiwa mtu mmoja mmoja; (b) kondoo wengine; (c) wasomaji wote wa vichapo vya Kikristo. Bwana-mkubwa aliweka mtumwa huyo juu ya mali yake yote katika mwaka wa (a) 1914; (b) 33 W.K.; (c) 1919.
14. Chagua Jibu Sahihi: Wavu unaozungumziwa katika mfano wa Yesu kwenye Mathayo 13: 47-50 umetia ndani kutaniko la Wakristo wapakwa-mafuta na (a) Ufalme wa Kimesiya wa Mungu; (b) waandamani wao wa kondoo wengine; (c) Jumuiya ya Wakristo.
15. Kulingana na maneno ya Yesu yanayopatikana kwenye Mathayo 5:24, unapaswa kufanya nini ikiwa unahisi kwamba umemuudhi mwabudu mwenzako? [g96-SW 2/8 uku. 26-7]