Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nehemia 4
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Nehemia—Yaliyomo

      • Kazi yaendelea licha ya upinzani (1-14)

      • Ujenzi waendelea wajenzi wakiwa na silaha (15-23)

Nehemia 4:1

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “aliudhika.”

Marejeo

  • +Ne 2:10; 6:1, 2; 13:28

Nehemia 4:2

Marejeo

  • +Ne 4:10

Nehemia 4:3

Marejeo

  • +Ne 2:19
  • +Ne 13:1, 2

Nehemia 4:4

Marejeo

  • +Zb 123:3
  • +Zb 79:12

Nehemia 4:5

Marejeo

  • +Yer 18:23

Nehemia 4:7

Marejeo

  • +Ne 4:3
  • +Ne 2:19
  • +Yos 13:2, 3; Ne 13:23

Nehemia 4:10

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Wabeba mizigo.”

Nehemia 4:12

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “mara kumi.”

Nehemia 4:14

Marejeo

  • +Ne 13:17
  • +Hes 14:9; Kum 20:3; Yos 1:9
  • +Kum 7:21; 10:17

Nehemia 4:16

Marejeo

  • +Ne 5:16
  • +Ne 11:1

Nehemia 4:18

Marejeo

  • +Hes 10:9; 2Nya 13:12

Nehemia 4:20

Marejeo

  • +Kum 1:30; Yos 23:10

Nehemia 4:23

Marejeo

  • +Ne 13:19

Jumla

Neh. 4:1Ne 2:10; 6:1, 2; 13:28
Neh. 4:2Ne 4:10
Neh. 4:3Ne 2:19
Neh. 4:3Ne 13:1, 2
Neh. 4:4Zb 123:3
Neh. 4:4Zb 79:12
Neh. 4:5Yer 18:23
Neh. 4:7Ne 4:3
Neh. 4:7Ne 2:19
Neh. 4:7Yos 13:2, 3; Ne 13:23
Neh. 4:14Ne 13:17
Neh. 4:14Hes 14:9; Kum 20:3; Yos 1:9
Neh. 4:14Kum 7:21; 10:17
Neh. 4:16Ne 5:16
Neh. 4:16Ne 11:1
Neh. 4:18Hes 10:9; 2Nya 13:12
Neh. 4:20Kum 1:30; Yos 23:10
Neh. 4:23Ne 13:19
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Nehemia 4:1-23

Nehemia

4 Mara tu Sanbalati+ aliposikia kwamba tunajenga upya ukuta, alishikwa na ghadhabu na kukasirika sana,* naye akazidi kuwadhihaki Wayahudi. 2 Akasema hivi mbele ya ndugu zake na jeshi la Samaria: “Wayahudi hawa wanyonge wanafanya nini? Je, watafanya kazi hii peke yao? Je, watatoa dhabihu? Je, watamaliza kwa siku moja? Je, watayatoa mawe yaliyoungua kutoka katika marundo ya vifusi ili yafae kwa ujenzi?”+

3 Basi Tobia+ Mwamoni,+ aliyekuwa amesimama kando yake, akasema: “Hata mbweha akipanda juu ya kile wanachojenga, atauangusha ukuta wao wa mawe.”

4 Sikiliza, Ee Mungu wetu, kwa maana tunadharauliwa;+ na urudishe dharau yao juu ya vichwa vyao wenyewe,+ nawe uwafanye wawe nyara na mateka katika nchi nyingine. 5 Usiifunike hatia yao wala usiifute dhambi yao kutoka mbele zako,+ kwa maana wamewatukana wajenzi.

6 Basi tukaendelea kujenga, na ukuta wote ukaungana kufikia nusu ya kimo chake, nao watu wakaendelea kufanya kazi kwa moyo wote.

7 Sasa mara tu Sanbalati, Tobia,+ Waarabu,+ Waamoni, na Waashdodi+ waliposikia kwamba kazi ya kurekebisha kuta za Yerusalemu inasonga mbele na kwamba mianya ilikuwa ikizibwa, wakakasirika sana. 8 Wakapanga njama pamoja ili kupigana na Yerusalemu na kuleta vurugu humo. 9 Lakini tulisali kwa Mungu wetu na kuweka walinzi dhidi yao mchana na usiku.

10 Hata hivyo, watu wa Yuda walikuwa wakisema: “Wafanyakazi* wameishiwa na nguvu, na kuna vifusi vingi sana; hatutafaulu kamwe kuujenga ukuta.”

11 Maadui wetu wakaendelea kusema: “Kabla hawajajua au kutuona, tutaingia kati yao, tuwaue, na kuikomesha kazi.”

12 Kila mara Wayahudi walioishi karibu nao walipokuja, walikuwa wakituambia tena na tena:* “Watatushambulia kutoka kila upande.”

13 Basi nikaweka wanaume kwenye sehemu za chini zaidi zilizo wazi nyuma ya ukuta, nikawapanga kulingana na familia zao, wakiwa na mapanga yao, mikuki yao, na pinde zao. 14 Nilipoona jinsi walivyoogopa, mara moja nikasimama na kuwaambia wakuu+ na watawala wasaidizi na watu wengine wote: “Msiwaogope.+ Mkumbukeni Yehova, ambaye ni mkuu na mwenye kuogopesha;+ nanyi mpigane kwa ajili ya ndugu zenu, wana wenu na mabinti zenu, wake zenu na nyumba zenu.”

15 Sasa baada ya maadui wetu kusikia kwamba tunajua walichokuwa wakifanya na kwamba Mungu wa kweli alikuwa amevuruga mpango wao, sote tukarudi kuujenga ukuta. 16 Tangu siku hiyo na kuendelea, nusu ya wanaume wangu walikuwa wakifanya kazi+ na nusu nyingine walikuwa wakishika mikuki, ngao, pinde, na kuvaa makoti ya vita. Na wakuu+ walisimama nyuma ya watu wote wa nyumba ya Yuda 17 waliokuwa wakijenga ukuta. Watu waliokuwa wakibeba mizigo walifanya kazi kwa mkono mmoja, huku wakiwa wameshika silaha kwa mkono mwingine. 18 Na kila mjenzi alikuwa amejifunga upanga kiunoni huku akijenga, na mtu wa kupiga pembe+ alikuwa amesimama kando yangu.

19 Ndipo nikawaambia wakuu na watawala wasaidizi na watu wengine wote: “Kazi hii ni kubwa na nzito, nasi tumetawanyika kwenye ukuta kila mmoja mbali na mwenzake. 20 Mtakaposikia mlio wa pembe, kusanyikeni mahali tulipo. Mungu wetu atatupigania.”+

21 Basi tukaendelea kufanya kazi huku nusu ya wanaume wakiwa wameshika mikuki, kuanzia mapambazuko mpaka nyota zilipoonekana. 22 Wakati huo nikawaambia watu: “Kila mwanaume na mtumishi wake na wakae ndani ya Yerusalemu usiku, nao watakuwa walinzi usiku na watafanya kazi mchana.” 23 Basi mimi, ndugu zangu, watumishi wangu,+ na walinzi waliofuatana nami hatukuvua mavazi yetu kamwe, na kila mmoja wetu aliendelea kushika silaha yake kwa mkono wa kulia.

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki