Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ayubu 13
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Ayubu—Yaliyomo

      • Ayubu aendelea kujibu (1-28)

        • ‘Ni afadhali nizungumze na Mungu’ (3)

        • ‘Ninyi ni matabibu wasiofaa kitu’ (4)

        • “Najua sina kosa” (18)

        • Auliza kwa nini Mungu anamwona kuwa adui (24)

Ayubu 13:3

Marejeo

  • +Ayu 23:3, 4; 31:35

Ayubu 13:4

Marejeo

  • +Ayu 16:2

Ayubu 13:5

Marejeo

  • +Met 17:28; Yak 1:19

Ayubu 13:8

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “mtampendelea.”

Ayubu 13:9

Marejeo

  • +Zb 139:23; Yer 17:10

Ayubu 13:10

Marejeo

  • +Zb 50:20, 21; Yak 2:9

Ayubu 13:12

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “inayokumbukwa.”

  • *

    Tnn., “Mafundo ya ngao zenu.”

Ayubu 13:14

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Kwa nini naubeba mwili wangu kwenye meno yangu?”

  • *

    Au “nafsi yangu.”

Ayubu 13:15

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Nitatetea njia zangu.”

Marejeo

  • +Ayu 19:25; Zb 23:4

Ayubu 13:16

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “mwasi imani.”

Marejeo

  • +Kut 15:2; Zb 27:1; Isa 12:2
  • +Ayu 27:8; 36:13; Isa 33:14

Ayubu 13:19

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “Ikiwa mtu anaweza kupambana nami, nitanyamaza na kufa.”

Ayubu 13:20

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Mambo mawili tu, usinitendee.”

Ayubu 13:21

Marejeo

  • +Ayu 9:34, 35; 33:6, 7

Ayubu 13:24

Marejeo

  • +Zb 10:1; 13:1; 44:24
  • +Ayu 16:9; 19:11; 33:8-11

Ayubu 13:28

Maelezo ya Chini

  • *

    Labda “mwanadamu” anayerejelewa ni Ayubu.

  • *

    Aina fulani ya mdudu mharibifu.

Jumla

Ayu. 13:3Ayu 23:3, 4; 31:35
Ayu. 13:4Ayu 16:2
Ayu. 13:5Met 17:28; Yak 1:19
Ayu. 13:9Zb 139:23; Yer 17:10
Ayu. 13:10Zb 50:20, 21; Yak 2:9
Ayu. 13:15Ayu 19:25; Zb 23:4
Ayu. 13:16Kut 15:2; Zb 27:1; Isa 12:2
Ayu. 13:16Ayu 27:8; 36:13; Isa 33:14
Ayu. 13:21Ayu 9:34, 35; 33:6, 7
Ayu. 13:24Zb 10:1; 13:1; 44:24
Ayu. 13:24Ayu 16:9; 19:11; 33:8-11
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
  • 27
  • 28
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Ayubu 13:1-28

Ayubu

13 “Naam, jicho langu limeona hayo yote,

Sikio langu limesikia na kuyaelewa.

 2 Mnayojua, mimi pia nayajua;

Mimi si duni kwenu.

 3 Lakini mimi, ni afadhali nizungumze na Mweza-Yote mwenyewe;

Ninatamani kujitetea mbele za Mungu.+

 4 Lakini ninyi mnanipaka uwongo;

Ninyi nyote ni matabibu wasiofaa kitu.+

 5 Laiti mngenyamaza kabisa,

Mngeonekana kuwa wenye hekima.+

 6 Tafadhali, sikilizeni hoja zangu,

Na msikilize ninapojitetea kwa midomo yangu.

 7 Je, mtasema mambo yasiyo ya haki kwa niaba ya Mungu,

Na je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa ajili yake?

 8 Je, mtamuunga mkono,*

Je, mtajaribu kumtetea Mungu wa kweli?

 9 Je, mambo yatawaendea vyema akiwachunguza?+

Je, mtamdanganya kama mnavyomdanganya mwanadamu anayeweza kufa?

10 Kwa hakika atawakemea

Mkijaribu kwa siri kuonyesha upendeleo.+

11 Je, adhama yake mwenyewe haitawaogopesha

Na hofu yake haitawaangukia?

12 Misemo yenu ya hekima* ni methali za majivu;

Kujitetea kwenu* ni hafifu kama ngome za udongo.

13 Nyamazeni mbele yangu, ili niongee.

Kisha na yanipate yatakayonipata!

14 Kwa nini ninajihatarisha*

Na kubeba uhai wangu* mikononi mwangu?

15 Hata akiniua, bado nitangoja;+

Nitajitetea* mbele zake.

16 Ndipo atakapokuwa wokovu wangu,+

Kwa maana hakuna mtu aliyemkataa Mungu* anayeweza kuja mbele zake.+

17 Sikilizeni kwa makini neno langu;

Sikilizeni tangazo langu.

18 Sasa tazameni, nimetayarisha kesi yangu;

Najua sina kosa.

19 Ni nani atakayepambana nami?

Nitakufa, ikiwa nitanyamaza!*

20 Ee Mungu, nifanyie mambo mawili tu,*

Ili nisijifiche kutoka mbele zako:

21 Ondoa mkono wako mzito uwe mbali nami,

Nawe usiache hofu yangu kukuelekea initishe.+

22 Niite nami nitakujibu,

Au acha nizungumze, nawe unijibu.

23 Nimefanya makosa na dhambi gani?

Nifunulie kosa langu na dhambi yangu.

24 Kwa nini unauficha uso wako+

Na kuniona kuwa adui yako?+

25 Je, utajaribu kulitisha jani linalopeperushwa na upepo

Au kuyakimbiza majani makavu?

26 Kwa maana unaendelea kuandika mashtaka makali dhidi yangu,

Nawe unanifanya niwajibike kwa sababu ya dhambi nilizofanya nilipokuwa kijana.

27 Umeitia miguu yangu katika mikatale,

Unavichunguza kwa makini vijia vyangu vyote,

Nawe unafuata kila wayo wa mguu wangu.

28 Kwa hiyo mwanadamu* huoza kama kitu kilichooza,

Kama vazi lililoliwa na nondo.*

Tanzanian sign language publications (2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki