Ayubu
3 Mwanadamu hulishinda giza;
Huchunguza kwa kina katika utusitusi na giza,
Akitafuta mawe yenye madini.
4 Huzamisha bomba mbali na makao ya watu,
Mahali paliposahauliwa, mbali na mahali ambapo watu wanatembea;
Wanaume fulani hushuka wakining’inia kwa kamba.
5 Chakula hukua juu ardhini;
Lakini chini, kuna msukosuko kama wa moto.*
6 Katika mawe hayo kuna yakuti,
Na vumbi lake lina dhahabu.
7 Hakuna ndege awindaye anayejua njia ya kufika huko;
Jicho la mwewe mweusi halijaiona.
8 Hakuna mnyama yeyote wa mwituni mwenye fahari aliyeikanyaga;
Mwanasimba hajazunguka huko.
9 Mwanadamu hugonga mwamba mgumu kwa mkono wake;
Huipindua milima kwenye misingi yake.
10 Huchimba mitaro ya maji+ kwenye mwamba;
Macho yake huona kila kitu chenye thamani.
11 Huziba chemchemi za mito
Na kufichua vitu vilivyofichwa.
13 Hakuna mwanadamu anayetambua thamani yake,+
Nayo haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai.
14 Vilindi vya maji vinasema, ‘Haimo ndani yangu!’
Nayo bahari inasema, ‘Haiko pamoja nami!’+
15 Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi;
Wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha.+
16 Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri+
Wala kwa madini ya shohamu na yakuti yasiyopatikana kwa urahisi.
17 Dhahabu na kioo haviwezi kulinganishwa nayo;
18 Marijani na fuwele hazistahili kutajwa,+
Kwa maana mfuko uliojaa hekima una thamani kuliko mfuko uliojaa lulu.
19 Topazi+ ya Kushi haiwezi kulinganishwa nayo;
Haiwezi kununuliwa hata kwa dhahabu safi.
20 Lakini hekima hutoka wapi,
Na kiko wapi chanzo cha uelewaji?+
21 Imefichwa kutoka machoni pa kila kiumbe aliye hai+
Na kufichwa kutoka kwa ndege wa angani.
22 Maangamizi na kifo husema,
‘Masikio yetu yamesikia tu habari zake.’
23 Mungu anaelewa njia ya kuipata;
Yeye peke yake ndiye anayejua inakokaa,+
24 Kwa maana yeye hutazama mpaka kwenye miisho ya dunia,
Naye huona kila kitu chini ya mbingu.+
Na kuyapima maji,+
26 Alipoiwekea mvua sheria+
Na njia kwa ajili ya mawingu ya dhoruba yenye ngurumo,+
27 Kisha akaiona hekima na kuifafanua;
Aliiimarisha na kuijaribu.
28 Naye akamwambia mwanadamu: