-
Kutoka 29:13, 14Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
13 Kisha chukua mafuta yote+ yanayofunika matumbo, mafuta yaliyo juu ya ini, na figo zake mbili na mafuta yaliyo juu yake, nawe uchome moto vitu hivyo ili vifuke moshi juu ya madhabahu.+ 14 Lakini nyama ya ng’ombe dume huyo na ngozi yake na mavi yake utaviteketeza nje ya kambi. Hiyo ni dhabihu ya dhambi.
-
-
Mambo ya Walawi 9:8Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
8 Haruni akaenda mara moja kwenye madhabahu na kumchinja yule ndama wa dhabihu ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe.+
-
-
Mambo ya Walawi 9:10Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
10 Akateketeza mafuta na figo na mafuta yaliyo juu ya ini kutoka katika dhabihu ya dhambi ili vifuke moshi kwenye madhabahu, kama Yehova alivyomwamuru Musa.+
-