Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutoka 15:23-25
    Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
    • 23 Wakafika Mara,*+ lakini hawakuweza kunywa maji ya Mara kwa sababu yalikuwa machungu. Ndiyo sababu alipaita mahali hapo Mara. 24 Basi watu wakaanza kumnung’unikia Musa,+ wakisema: “Tutakunywa nini?” 25 Musa akamlilia Yehova,+ naye Yehova akamwelekeza kwenye mti fulani. Alipoutupa ndani ya maji hayo, yakawa matamu.

      Huko Mungu akawawekea sharti na msingi wa hukumu, na huko Mungu akawajaribu.+

  • 2 Wafalme 4:38-41
    Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
    • 38 Elisha aliporudi Gilgali, kulikuwa na njaa kali nchini.+ Wana wa manabii+ walikuwa wameketi mbele yake, akamwambia mtumishi wake:+ “Weka kile chungu kikubwa motoni uwachemshie mchuzi wana wa manabii.” 39 Basi mmoja wao akaenda shambani kuchuma miholi, akapata mzabibu wa mwituni na kuchuma maboga ya mwituni kutoka kwenye mzabibu huo, akajaza vazi lake. Kisha akarudi na kuyakata vipandevipande ndani ya chungu cha mchuzi, bila kujua yalikuwa nini. 40 Baadaye wakawapakulia wanaume hao ili wale, lakini mara tu walipokunywa mchuzi huo, wakalia wakisema: “Kuna kifo ndani ya chungu hiki, Ee mtu wa Mungu wa kweli.” Nao hawakuweza kuunywa. 41 Kwa hiyo Elisha akasema: “Leteni unga kidogo.” Baada ya kuutupa ndani ya chungu hicho, akasema: “Wapakulieni watu.” Na hakukuwa tena na kitu chochote chenye kudhuru ndani ya chungu hicho.+

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki