-
2 Wafalme 22:18, 19Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
18 Lakini mwambieni hivi mfalme wa Yuda aliyewatuma kutafuta ushauri wa Yehova: “Yehova Mungu wa Israeli anasema hivi: ‘Kuhusu maneno ambayo umesikia, 19 kwa sababu moyo wako ulikuwa msikivu,* nawe ukajinyenyekeza+ mbele za Yehova uliposikia mambo niliyosema dhidi ya mahali hapa na wakaaji wake—kwamba watakuwa kitu cha kutisha na laana—nawe ukayararua mavazi yako+ na kulia mbele zangu, mimi pia nimekusikia, asema Yehova.
-
-
Luka 15:22-24Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
22 Lakini baba yake akawaambia watumwa, ‘Leteni upesi kanzu bora zaidi na kumvika, pia mvisheni pete mkononi na viatu miguuni. 23 Vilevile, leteni ndama aliyenoneshwa, mchinjeni, nasi tule na tusherehekee, 24 kwa sababu huyu mwanangu alikuwa amekufa na sasa yuko hai;+ alikuwa amepotea naye amepatikana.’ Basi wakaanza kusherehekea.
-