Tafsiri ya Ulimwegu Mpya 2 Samweli—Yaliyomo 2 SAMWELI YALIYOMO 1 Daudi apata habari za kifo cha Sauli (1-16) Daudi aimba wimbo wa kumwombolezea Sauli na Yonathani (17-27) 2 Daudi, mfalme wa Yuda (1-7) Ish-boshethi, mfalme wa Israeli (8-11) Vita kati ya nyumba ya Daudi na nyumba ya Sauli (12-32) 3 Nyumba ya Daudi yazidi kupata nguvu (1) Wana wa Daudi (2-5) Abneri ajiunga na Daudi (6-21) Yoabu amuua Abneri (22-30) Daudi amwombolezea Abneri (31-39) 4 Ish-boshethi auawa (1-8) Daudi aagiza waliomuua Ish-boshethi wauawe (9-12) 5 Daudi awekwa kuwa mfalme wa nchi yote ya Israeli (1-5) Yerusalemu latekwa (6-16) Sayuni, Jiji la Daudi (7) Daudi awashinda Wafilisti (17-25) 6 Sanduku la agano laletwa Yerusalemu (1-23) Uza alikamata sanduku la agano na kuuawa (6-8) Mikali amdharau Daudi (16, 20-23) 7 Daudi hatajenga hekalu (1-7) Agano pamoja na Daudi kwa ajili ya ufalme (8-17) Sala ya Daudi ya shukrani (18-29) 8 Ushindi mbalimbali wa Daudi (1-14) Wakuu katika utawala wa Daudi (15-18) 9 Daudi amtendea Mefiboshethi kwa upendo mshikamanifu (1-13) 10 Awashinda Waamoni na Wasiria (1-19) 11 Daudi afanya uzinzi na Bath-sheba (1-13) Daudi apanga Uria auawe (14-25) Daudi amchukua Bath-sheba kuwa mke wake (26, 27) 12 Nathani amkaripia Daudi (1-15a) Mwana wa Bath-sheba afa (15b-23) Bath-sheba amzaa Sulemani (24, 25) Jiji la Raba la Waamoni latekwa (26-31) 13 Amnoni ambaka Tamari (1-22) Absalomu amuua Amnoni (23-33) Absalomu akimbilia Geshuri (34-39) 14 Yoabu na mwanamke Mtekoa (1-17) Daudi agundua njama ya Yoabu (18-20) Absalomu aruhusiwa kurudi (21-33) 15 Njama na uasi wa Absalomu (1-12) Daudi akimbia kutoka Yerusalemu (13-30) Ahithofeli ajiunga na Absalomu (31) Hushai atumwa kuvuruga ushauri wa Ahithofeli (32-37) 16 Siba amchongea Mefiboshethi (1-4) Shimei amtukana Daudi (5-14) Absalomu ampokea Hushai (15-19) Ushauri wa Ahithofeli (20-23) 17 Hushai avuruga ushauri wa Ahithofeli (1-14) Daudi aonywa; amtoroka Absalomu (15-29) Barzilai na wengine wamletea vyakula (27-29) 18 Absalomu ashindwa; kifo chake (1-18) Daudi ajulishwa kuhusu kifo cha Absalomu (19-33) 19 Daudi amwombolezea Absalomu (1-4) Yoabu amkaripia Daudi (5-8a) Daudi arudi Yerusalemu (8b-15) Shimei aomba msamaha (16-23) Mefiboshethi athibitishwa kuwa hana hatia (24-30) Barzilai aheshimiwa (31-40) Makabila yazozana (41-43) 20 Uasi wa Sheba; Yoabu amuua Amasa (1-13) Sheba afuatwa na kukatwa kichwa (14-22) Wakuu katika utawala wa Daudi (23-26) 21 Nyumba ya Sauli yalipizwa kisasi kwa ajili ya Wagibeoni (1-14) Vita dhidi ya Wafilisti (15-22) 22 Daudi amsifu Mungu kwa sababu ya matendo yake ya wokovu (1-51) “Yehova ni jabali langu” (2) Yehova ni mshikamanifu kwa walio washikamanifu (26) 23 Maneno ya mwisho ya Daudi (1-7) Mambo yaliyotendwa na mashujaa hodari wa Daudi (8-39) 24 Dhambi ya Daudi ya kuwahesabu watu (1-14) Ugonjwa hatari wasababisha vifo vya watu 70,000 (15-17) Daudi ajenga madhabahu (18-25) Hatatoa dhabihu ambazo hazimgharimu (24)