WIMBO NA. 34
Kutembea kwa Utimilifu
- 1. Nihukumu, Nakutumaini; - Na utimilifu wangu uchunguze. - Nichunguze na unijaribu; - Nisafishe moyo, na unibariki. - (KORASI) - Ee Yehova, Nimeazimia - Kuwa mwaminifu, siku zangu zote. 
- 2. Sikuketi na wadanganyifu. - Nimelichukia kundi la waovu. - Tafadhali usiniharibu, - Pamoja na watu wapendao rushwa. - (KORASI) - Ee Yehova, Nimeazimia - Kuwa mwaminifu, siku zangu zote. 
- 3. Nyumba yako naipenda sana. - Na ibada yako, naitanguliza. - Nizunguke madhabahu yako, - Nitangaze kote kazi zako zote. - (KORASI) - Ee Yehova, Nimeazimia - Kuwa mwaminifu, siku zangu zote. 
(Ona pia Zab. 25:2.)