WIMBO NA. 35
“Mhakikishe Mambo Muhimu Zaidi”
- 1. Twahitaji utambuzi, - Kujua mambo yafaayo, - Ambayo ni muhimu zaidi - Tupasayo kufanya! - (KORASI) - Penda mema; Mungu wetu - Afurahi. - Tuchukie mabaya. Tusali - Na kufanya - Yaliyo muhimu zaidi. 
- 2. Nini kingine chenye maana - Kuliko kuhubiri? - Na kutafuta kondoo wa - Mungu waliopotea? - (KORASI) - Penda mema; Mungu wetu - Afurahi. - Tuchukie mabaya. Tusali - Na kufanya - Yaliyo muhimu zaidi. 
- 3. Tukifanya yaliyo muhimu, - Tutapata uradhi. - Na amani ya akili - Ipitayo zote tupate. - (KORASI) - Penda mema; Mungu wetu - Afurahi. - Tuchukie mabaya. Tusali - Na kufanya - Yaliyo muhimu zaidi. 
(Ona pia Zab. 97:10; Yoh. 21:15-17; Flp. 4:7.)