WIMBO NA. 56
Fanya Kweli Iwe Njia Yako ya Maisha
- 1. Njia ya kweli, ni njia bora sana, - Uamuzi ni wako wewe. - Na mashauri ya Yehova utii; - Umtumaini Yeye. - (KORASI) - Shika ukweli. - Kwako uwe halisi. - Utapata shangwe - ya Yehova - Ukishika ukweli. 
- 2. Bidii yako, na jitihada zako, - Katika kazi ya Ufalme, - Zitatokeza baraka za milele, - Na tumaini jangavu. - (KORASI) - Shika ukweli. - Kwako uwe halisi. - Utapata shangwe - ya Yehova - Ukishika ukweli. 
- 3. Kama watoto, twahitaji mwongozo, - Mashauri na mwelekezo. - Na tutembee kila siku na Mungu; - Tupate baraka zake. - (KORASI) - Shika ukweli. - Kwako uwe halisi. - Utapata shangwe - ya Yehova - Ukishika ukweli. 
(Ona pia Zab. 26:3; Met. 8:35; 15:31; Yoh. 8:31, 32.)