WIMBO NA. 144
Kaza Macho Kwenye Zawadi!
- 1. Watakapoona vipofu, - Nao viziwi wasikie, - Watoto watakapoimba, - Amani, shangwe ziwepo, - Wapendwa watafufuliwa, - Na kuishi pasipo dhambi. - (KORASI) - Utayaona mambo hayo, - Ukitazama zawadi. 
- 2. Mbwa-mwitu, mwanakondoo - Watakula nyasi pamoja, - Naye mvulana mdogo, - Atawaongoza wote. - Hakutakuwa na machozi, - Mwisho wa maumivu, hofu. - (KORASI) - Utayaona mambo hayo, - Ukitazama zawadi. 
(Ona pia Isa. 11:6-9; 35:5-7; Yoh. 11:24.)