WIMBO NA. 38
Atakupa Nguvu
- 1. Kweli yake Mungu amekufundisha, - Amekutoa katika giza. - Aliona moyo wako watamani, - Kufanya mambo yaliyo mema. - Kwa sala ulijiweka wakfu; - Daima atakuimarisha. - (KORASI) - Kwa damu ya Mwanaye, - alikununua. - Hukuimarisha, - na kukupa nguvu. - Atakulinda na - kukuongoza wewe. - Hukuimarisha, - na kukupa nguvu. 
- 2. Katoa Mwanaye, kwa niaba yako; - Hivyo, ataka ufanikiwe. - Basi kama Mungu alifanya hivyo, - Bila shaka atakupa nguvu. - Imani yako hatasahau; - Walio wake atawatunza. - (KORASI) - Kwa damu ya Mwanaye, - alikununua. - Hukuimarisha, - na kukupa nguvu. - Atakulinda na - kukuongoza wewe. - Hukuimarisha, - na kukupa nguvu. 
(Ona pia Rom. 8:32; 14:8, 9; Ebr. 6:10; 1 Pet. 2:9.)