WIMBO NA. 58
Kutafuta Marafiki wa Amani
- 1. Yesu kaweka kielelezo, - Kwa kutangaza Ufalme, - Popote alipokuwa. - Aliwapenda kondoo wote. - Siku nzima hakuchoka - hadi usiku. - Milangoni na njiani, - Tunazo habari njema, - U karibu mwisho wa matatizo. - (KORASI) - Twatafuta - Kote rafiki wa amani. - Twatafuta - Moyo utakao wokovu. - Twahubiri - Kotekote. 
- 2. Hatuna muda wa kupoteza. - Mamilioni ya watu, - Wako hatarini leo. - Upendo wetu hutuchochea. - Kufariji watu wote, - Na kuwafunza. - Vijijini na mijini, - Astahilipo mmoja, - Kwa pamoja sote twashangilia. - (KORASI) - Twatafuta - Kote rafiki wa amani. - Twatafuta - Moyo utakao wokovu. - Twahubiri - Kotekote. 
(Ona pia Isa. 52:7; Mt. 28:19, 20; Luka 8:1; Rom. 10:10.)