WIMBO NA. 95
Nuru Inazidi Kuongezeka
- 1. Kale manabii walitabiri - Kristo tumaini la wote. - Roho ya Yehova ilifunua, - Masihi angewakomboa. - Sasa Kristo Yesu anatawala - Ishara zinaonyesha. - Tuna pendeleo kujua hayo, - Malaika huchungulia! - (KORASI) - Nuru inazidi kung’aa; - Twatembea kwenye nuru. - Yehova atufunulia; - Aongoza njia zetu. 
- 2. Yesu ametupa mtumwa wake, - Anayetulisha kiroho. - Na nuru ya kweli yaongezeka - Inatuchochea mioyo. - Njia yetu yaonekana wazi - Twatembea kwenye nuru. - Asante Yehova! Chanzo cha kweli, - Asante kwa kutuongoza. - (KORASI) - Nuru inazidi kung’aa; - Twatembea kwenye nuru. - Yehova atufunulia; - Aongoza njia zetu. 
(Ona pia Rom. 8:22; 1 Kor. 2:10; 1 Pet. 1:12.)