Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb25 Septemba kur. 4-5
  • Septemba 15-21

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Septemba 15-21
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2025
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2025
mwb25 Septemba kur. 4-5

SEPTEMBA 15-21

METHALI 31

Wimbo 135 na Sala | Utangulizi (Dak. 1)

HAZINA ZA NENO LA MUNGU

Mama akizungumza na binti yake kwa uchangamfu huku wakiwa wameketi kwenye kochi.

1. Masomo Tunayojifunza Kutokana na Maagizo ya Mama Mwenye Upendo

(Dak. 10)

Wafundishe watoto wako maoni ya Yehova kuhusu ngono na ndoa (Met 31:​3, 10; w11 2/1 19 ¶7-8)

Wafundishe watoto wako wawe na maoni kama ya Yehova kuhusu kileo (Met 31:​4-6; ijwhf makala ya 4 ¶11-13)

Wafundishe watoto wako kuwasaidia watu kama Yehova anavyofanya (Met 31:​8, 9; g17.6 9 ¶5)

2. Hazina za Kiroho

(Dak. 10)

  • Met 31:​10-31—Herufi za kialfabeti ni nini, na zilitumiwaje katika Maandiko ya Kiebrania? (w92 11/1 11 ¶7-8)

  • Ungependa kushiriki nasi hazina gani kutoka kwenye usomaji wa Biblia wa juma hili?

3. Usomaji wa Biblia

(Dak. 4) Met 31:​10-31 (th somo la 10)

BORESHA HUDUMA YAKO

4. Kuanzisha Mazungumzo

(Dak. 3) MAHUBIRI YASIYO RASMI. Anzisha mazungumzo na mtu ambaye amesema au kutenda jambo fulani la fadhili. (lmd somo la 5 jambo kuu la 3)

5. Kuanzisha Mazungumzo

(Dak. 4) NYUMBA KWA NYUMBA. Zungumzia moja ya “Kweli Tunazopenda Kufundisha” kutoka kwenye nyongeza A ya broshua Wapende Watu. (lmd somo la 1 jambo kuu la 4)

6. Kufuatia Upendezi

(Dak. 5) NYUMBA KWA NYUMBA. Mwalike mwenye nyumba ambaye ulimwachia gazeti la Mnara wa Mlinzi Na. 1 2025 ahudhurie hotuba ya pekee. (lmd somo la 7 jambo kuu la 4)

MAISHA YA MKRISTO

Wimbo 121

7. Wafundishe Watoto Wako Kutumia Vifaa vya Kielektroni kwa Hekima

(Dak. 8) Mazungumzo.

Je, umewahi kumtazama mtoto mdogo akitumia programu za simu ya mkononi au tablet? Mara nyingi, inaonekana ni rahisi sana kwa watoto kutumia vifaa hivyo! Huenda wasihitaji msaada wa kujua jinsi ya kutumia vifaa, lakini sikuzote watahitaji kujifunza jinsi ya kuvitumia kwa hekima. Ikiwa wewe ni mzazi, unawezaje kumzoeza mtoto wako kutumia kifaa cha kielektroni kwa hekima?

Kisehemu kutoka kwenye video “Kutumia Wakati Vizuri.” Sophia anatumia tablet yake akiwa ameketi ufuoni, na anakosa kuwaona pomboo wanaochezea mpira kwenye maji yaliyo hapo karibu.

Onyesha VIDEO Kutumia Wakati Vizuri. Kisha waulize wasikilizaji:

  • Kwa nini ni vizuri kujiwekea mipaka tunapotumia vifaa vya kielektroni?

  • Tunahitaji kutenga wakati kwa ajili ya mambo gani mengine?

Unapoweka sheria kwa ajili ya familia yako, tegemea kanuni za Biblia badala ya kutegemea kile ambacho wazazi wengine hufanya. (Gal 6:5) Kwa mfano, jiulize:

  • Je, mtoto wangu ameonyesha kwamba ana sifa ya kujizuia na kuwajibika kwa matendo yake vya kutosha hivi kwamba anaweza kutumia kifaa changu au hata kuwa na kifaa chake cha kielektroni?—1Ko 9:25

  • Ninapaswa kumsimamia mtoto wangu kwa kadiri gani anapotumia kifaa cha kielektroni?—Met 18:1

  • Ni programu gani za simu au tovuti nitakazomruhusu mtoto wangu kutumia na ni zipi ambazo sitamruhusu atumie?—Efe 5:​3-5; Flp 4:​8, 9

  • Ninapaswa kumruhusu mtoto atumie muda gani kwenye kifaa cha kielektroni kwa siku, ili pia awe na muda wa kutosha wa kufanya mambo yenye kufurahisha na yaliyo muhimu?—Mhu 3:1

8. Mahitaji ya Kutaniko

(Dak. 7)

9. Funzo la Biblia la Kutaniko

(Dak. 30) lfb somo la 18-19

Umalizio (Dak. 3) | Wimbo 2 na Sala

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki