Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwanzo 23
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Mwanzo—Yaliyomo

      • Kifo cha Sara na mahali alipozikwa (1-20)

Mwanzo 23:1

Marejeo

  • +Mwa 17:17

Mwanzo 23:2

Marejeo

  • +Yos 14:15
  • +Mwa 35:27; Hes 13:22
  • +Mwa 12:5

Mwanzo 23:3

Marejeo

  • +Mwa 10:15

Mwanzo 23:4

Marejeo

  • +Mwa 17:1, 8; Ebr 11:9, 13

Mwanzo 23:6

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “kiongozi mkuu.”

Marejeo

  • +Mwa 21:22

Mwanzo 23:7

Marejeo

  • +1Nya 1:13

Mwanzo 23:9

Marejeo

  • +Mwa 23:15
  • +Mwa 25:9, 10; 49:29-33; 50:13, 14

Mwanzo 23:10

Marejeo

  • +Ru 4:1

Mwanzo 23:15

Maelezo ya Chini

  • *

    Shekeli moja ilikuwa na uzito wa gramu 11.4. Angalia Nyongeza B14.

Mwanzo 23:16

Maelezo ya Chini

  • *

    Shekeli moja ilikuwa na uzito wa gramu 11.4. Angalia Nyongeza B14.

Marejeo

  • +Mdo 7:15, 16

Mwanzo 23:20

Marejeo

  • +Mwa 25:9, 10; 49:29-33; 50:13, 14

Jumla

Mwa. 23:1Mwa 17:17
Mwa. 23:2Yos 14:15
Mwa. 23:2Mwa 35:27; Hes 13:22
Mwa. 23:2Mwa 12:5
Mwa. 23:3Mwa 10:15
Mwa. 23:4Mwa 17:1, 8; Ebr 11:9, 13
Mwa. 23:6Mwa 21:22
Mwa. 23:71Nya 1:13
Mwa. 23:9Mwa 23:15
Mwa. 23:9Mwa 25:9, 10; 49:29-33; 50:13, 14
Mwa. 23:10Ru 4:1
Mwa. 23:16Mdo 7:15, 16
Mwa. 23:20Mwa 25:9, 10; 49:29-33; 50:13, 14
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Mwanzo 23:1-20

Mwanzo

23 Na Sara aliishi miaka 127; hiyo ndiyo iliyokuwa miaka ya maisha ya Sara.+ 2 Basi Sara akafa huko Kiriath-arba,+ yaani, Hebroni,+ katika nchi ya Kanaani,+ naye Abrahamu akaanza kumwombolezea Sara na kumlilia. 3 Kisha Abrahamu akainuka na kutoka mahali ambapo maiti ya mke wake ilikuwepo, akawaambia wana wa Hethi:+ 4 “Mimi ni mgeni na mhamiaji miongoni mwenu.+ Nipeni ardhi ya kuzikia miongoni mwenu ili niweze kuwazika watu wangu waliokufa.” 5 Ndipo wana wa Hethi wakamwambia Abrahamu: 6 “Tusikilize, bwana wetu. Wewe ni kiongozi aliyechaguliwa na Mungu* miongoni mwetu.+ Unaweza kuwazika watu wako waliokufa mahali bora zaidi katika maeneo yetu ya kuzikia. Hakuna yeyote kati yetu atakayekunyima mahali pa kuwazika watu wako waliokufa.”

7 Basi Abrahamu akasimama na kuinama mbele ya wenyeji wa nchi, wana wa Hethi,+ 8 akawaambia: “Ikiwa mmekubali nimzike mtu wangu aliyekufa, basi nisikilizeni na mumsihi Efroni mwana wa Zohari 9 aniuzie pango lake la Makpela; liko ukingoni mwa shamba lake. Na aniuzie mbele yenu kwa kiasi kamili cha fedha+ ili niwe na mahali pa kuwazikia watu wangu.”+

10 Sasa Efroni alikuwa ameketi kati ya wana wa Hethi. Kwa hiyo Efroni Mhiti akamjibu Abrahamu mbele ya wana wa Hethi, na mbele ya wote walioingia katika lango la jiji,+ akasema: 11 “Hapana, bwana wangu! Nisikilize. Ninakupa shamba hilo pamoja na pango lililomo. Ninakupa mbele ya wana wa watu wangu. Mzike mtu wako aliyekufa.” 12 Ndipo Abrahamu akainama chini mbele ya wenyeji wa nchi 13 na kumwambia hivi Efroni mbele ya watu: “Tafadhali, nisikilize! Nitakupa kiasi kamili cha fedha kwa ajili ya shamba hilo. Zichukue kutoka mikononi mwangu, ili nimzike humo mtu wangu aliyekufa.”

14 Kisha Efroni akamwambia Abrahamu: 15 “Bwana wangu, nisikilize. Thamani ya shamba hili ni shekeli 400 za fedha,* lakini hiyo ni nini kati yangu na wewe? Mzike mtu wako aliyekufa.” 16 Abrahamu akamsikiliza Efroni, na Abrahamu akampimia Efroni kiasi cha fedha alichokuwa amemtajia mbele ya wana wa Hethi, shekeli 400 za fedha* kulingana na uzito uliokubaliwa na wafanyabiashara.+ 17 Kwa hiyo shamba la Efroni lililokuwa Makpela, mbele ya Mamre—shamba na pango lililokuwemo na miti yote iliyokuwa ndani ya mipaka ya shamba hilo—likathibitishwa kuwa 18 mali ya Abrahamu aliyoinunua mbele ya wana wa Hethi, mbele ya wote walioingia katika lango la jiji lake. 19 Baada ya hayo Abrahamu akamzika Sara mke wake katika pango la shamba la Makpela mbele ya Mamre, yaani, Hebroni, katika nchi ya Kanaani. 20 Hivyo wana wa Hethi wakamkabidhi Abrahamu lile shamba pamoja na pango lililokuwemo ili awazike watu wake humo.+

Tanzanian sign language publications (2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki