Ayubu
11 Sofari+ Mnaamathi akajibu:
2 “Je, maneno haya yote yatakosa kujibiwa,
Au kuongea mengi kutamfanya mtu asiwe na kosa?*
3 Je, maneno yako yasiyo na maana yatawanyamazisha watu?
Unadhani hakuna atakayekukemea kwa sababu ya maneno yako ya dhihaka?+
5 Lakini laiti Mungu angezungumza
Na kukufungulia midomo yake!+
6 Ndipo angekufunulia siri za hekima,
Kwa maana hekima inayotumika ina vipengele vingi.
Kisha ungetambua kwamba Mungu huruhusu baadhi ya makosa yako yasahauliwe.
7 Je, unaweza kugundua mambo ya Mungu yenye kina
Au kugundua kila jambo kumhusu* Mweza-Yote?
8 Hekima yake iko juu kuliko mbingu. Wewe unaweza kutimiza nini?
Ina kina kuliko Kaburi.* Wewe unaweza kujua nini?
9 Ni ndefu kuliko dunia
Na pana kuliko bahari.
10 Akipita na kumkamata mtu na kuweka kikao cha mahakama,
Ni nani anayeweza kumpinga?
11 Kwa maana anajua watu wanapokuwa wadanganyifu.
Akiona uovu, je, hatautambua?
12 Lakini mtu asiye na akili ataelewa
Wakati tu punda mwitu atakapoweza kuzaa mwanadamu.*
13 Laiti ungeutayarisha moyo wako
Na kumnyooshea mikono yako.
14 Ikiwa mkono wako unatenda mabaya, utupilie mbali,
Nawe usiruhusu uovu ukae katika mahema yako.
15 Ndipo utakapoinua uso wako bila lawama;
Utaweza kusimama imara, bila woga.
16 Ndipo utakapoisahau taabu yako;
Utaikumbuka kama maji yaliyopita karibu nawe na kwenda zake.
17 Maisha yako yatang’aa kuliko adhuhuri;
Hata giza lake litakuwa kama asubuhi.
18 Utakuwa na ujasiri kwa sababu kuna tumaini,
Nawe utatazama huku na huku na kulala kwa usalama.
19 Utalala na hakuna yeyote atakayekuogopesha,
Na watu wengi watajipendekeza kwako.
20 Lakini macho ya waovu yatadhoofika;
Nao hawatapata mahali pa kukimbilia,
Na tumaini lao pekee litakuwa kifo.”+