Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ayubu 19
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Ayubu—Yaliyomo

      • Jibu la Ayubu (1-29)

        • Akataa kukemewa na “rafiki” zake (1-6)

        • Asema kwamba ameachwa (13-19)

        • “Mkombozi wangu yuko hai” (25)

Ayubu 19:2

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “kuikasirisha nafsi yangu.” Angalia Kamusi.

Marejeo

  • +Zb 42:10
  • +Zb 55:21; Met 12:18

Ayubu 19:3

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Mmenitukana.”

Marejeo

  • +Met 18:24

Ayubu 19:7

Marejeo

  • +Zb 22:2; Hab 1:2
  • +Lu 18:7

Ayubu 19:8

Marejeo

  • +Ayu 3:23; Zb 88:8

Ayubu 19:11

Marejeo

  • +Ayu 13:24

Ayubu 19:13

Marejeo

  • +Zb 31:11; 69:8

Ayubu 19:14

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Watu wangu wa ukoo.”

Marejeo

  • +Zb 38:11

Ayubu 19:15

Marejeo

  • +Ayu 31:32

Ayubu 19:17

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “wana wa tumbo langu la uzazi,” yaani, tumbo lililonibeba (tumbo la mama yangu).

Marejeo

  • +Ayu 2:9

Ayubu 19:19

Marejeo

  • +Ayu 17:6; Zb 88:8
  • +Zb 109:5

Ayubu 19:20

Marejeo

  • +Ayu 30:30; Zb 102:5

Ayubu 19:21

Marejeo

  • +Ayu 1:10-12; Zb 38:2

Ayubu 19:22

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Na hamtosheki na mwili wangu?”

Marejeo

  • +Ayu 2:9, 10
  • +Zb 69:26

Ayubu 19:25

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “juu ya (kwenye) mavumbi.”

Marejeo

  • +Ayu 14:14; Zb 19:14; 69:18; 103:2, 4; Mt 20:28; Mk 10:45

Ayubu 19:27

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Figo zangu zimeacha kufanya kazi.”

Marejeo

  • +Zb 17:15

Ayubu 19:28

Marejeo

  • +Zb 69:26

Ayubu 19:29

Marejeo

  • +Kum 32:41
  • +Zb 58:11; Mt 7:1; Ro 14:4; Yak 4:12

Jumla

Ayu. 19:2Zb 42:10
Ayu. 19:2Zb 55:21; Met 12:18
Ayu. 19:3Met 18:24
Ayu. 19:7Zb 22:2; Hab 1:2
Ayu. 19:7Lu 18:7
Ayu. 19:8Ayu 3:23; Zb 88:8
Ayu. 19:11Ayu 13:24
Ayu. 19:13Zb 31:11; 69:8
Ayu. 19:14Zb 38:11
Ayu. 19:15Ayu 31:32
Ayu. 19:17Ayu 2:9
Ayu. 19:19Ayu 17:6; Zb 88:8
Ayu. 19:19Zb 109:5
Ayu. 19:20Ayu 30:30; Zb 102:5
Ayu. 19:21Ayu 1:10-12; Zb 38:2
Ayu. 19:22Ayu 2:9, 10
Ayu. 19:22Zb 69:26
Ayu. 19:25Ayu 14:14; Zb 19:14; 69:18; 103:2, 4; Mt 20:28; Mk 10:45
Ayu. 19:27Zb 17:15
Ayu. 19:28Zb 69:26
Ayu. 19:29Kum 32:41
Ayu. 19:29Zb 58:11; Mt 7:1; Ro 14:4; Yak 4:12
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
  • 27
  • 28
  • 29
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Ayubu 19:1-29

Ayubu

19 Ayubu akajibu:

 2 “Mtaendelea kunikasirisha* mpaka lini,+

Na kuniponda kwa maneno?+

 3 Mmenikemea* mara kumi sasa;

Mnanitesa bila aibu.+

 4 Na ikiwa kwa kweli nilifanya kosa,

Ni kosa langu mimi mwenyewe.

 5 Ikiwa mnasisitiza kujikweza juu yangu,

Mkidai kwamba mna haki ya kunishutumu,

 6 Basi, jueni kwamba Mungu ndiye amenipotosha,

Naye ameninasa katika wavu wake wa kuwindia.

 7 Tazameni! Naendelea kulia kwa sauti, ‘Ukatili!’ lakini sijibiwi;+

Naendelea kulilia msaada, lakini hakuna haki.+

 8 Ameziba kijia changu kwa ukuta wa mawe, siwezi kupita;

Amezifunika njia zangu kwa giza.+

 9 Amenivua utukufu wangu

Na kunivua taji kichwani.

10 Hunibomoa kila upande na kuniangamiza;

Anang’oa tumaini langu kama mti.

11 Hasira yake huwaka dhidi yangu,

Naye huniona kuwa adui yake.+

12 Majeshi yake hukusanyika na kunizingira,

Nayo hupiga kambi kuzunguka hema langu.

13 Ndugu zangu wenyewe amewafukuza mbali nami,

Na wale wanaonijua wamegeuka na kuniacha.+

14 Rafiki zangu wa karibu* wametoweka,

Na wale niliowajua vema wamenisahau.+

15 Wageni walio nyumbani mwangu+ na vijakazi wangu wananiona kuwa mgeni;

Mimi ni mgeni machoni pao.

16 Ninamwita mtumishi wangu, lakini hajibu;

Namsihi kwa kinywa changu anihurumie.

17 Pumzi yangu mwenyewe inamchukiza mke wangu,+

Nami ni uvundo kwa ndugu* zangu wenyewe.

18 Hata watoto wachanga wananidharau;

Ninaposimama, wanaanza kunifanyia mzaha.

19 Rafiki zangu wote wa karibu wananichukia,+

Na wale niliowapenda wamenigeuka.+

20 Mifupa yangu inashikamana na ngozi yangu na mwili wangu,+

Nami ninaponyoka kwa ngozi ya meno yangu.

21 Nionyesheni rehema, rafiki zangu, nionyesheni rehema,

Kwa maana mkono wa Mungu mwenyewe umenigusa.+

22 Kwa nini mnaendelea kunitesa kama Mungu anavyonitesa,+

Mkinishambulia bila kuacha?*+

23 Laiti maneno yangu yangeandikwa,

Laiti yangeandikwa katika kitabu!

24 Laiti yangechongwa milele kwenye mwamba,

Kwa kalamu ya chuma na risasi!

25 Kwa maana najua vizuri kwamba mkombozi wangu+ yuko hai;

Atakuja baadaye na kuinuka juu ya dunia.*

26 Baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi,

Nikiwa bado hai, nitamwona Mungu,

27 Ambaye mimi mwenyewe nitamwona,

Ambaye macho yangu mwenyewe yatamwona, si ya mwingine.+

Lakini ndani kabisa ninahisi nimelemewa!*

28 Kwa maana mnauliza, ‘Tunamtesa kwa njia gani?’+

Kwa maana mimi ndiye mzizi wa tatizo hili.

29 Ninyi wenyewe ogopeni upanga,+

Kwa kuwa upanga huwaadhibu wakosaji;

Mnapaswa kujua kwamba kuna mwamuzi.”+

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki