Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Isaya 18
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Isaya—Yaliyomo

      • Ujumbe dhidi ya Ethiopia (1-7)

Isaya 18:1

Marejeo

  • +Isa 20:3, 4; Eze 30:4

Isaya 18:2

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “taifa lenye watu waliochomoza juu na kusuguliwa.”

  • *

    Au “taifa lenye nguvu nyingi linaloyakanyaga mataifa mengine.”

Marejeo

  • +2Nya 12:2, 3; 14:9; 16:8

Isaya 18:3

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “nguzo ya ishara.”

Isaya 18:4

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “kutazama kutoka.”

Isaya 18:7

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “taifa lenye watu waliochomoza juu na kusuguliwa.”

  • *

    Au “taifa lenye nguvu nyingi linaloyakanyaga mataifa mengine.”

Marejeo

  • +Isa 8:18; 24:23

Jumla

Isa. 18:1Isa 20:3, 4; Eze 30:4
Isa. 18:22Nya 12:2, 3; 14:9; 16:8
Isa. 18:7Isa 8:18; 24:23
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Isaya 18:1-7

Isaya

18 Ole wa nchi ya wadudu wenye mabawa yanayovuma

Katika eneo la mito ya Ethiopia!+

 2 Inatuma wajumbe kupitia baharini,

Wanaovuka maji katika vyombo vya mafunjo, ikisema:

“Nendeni, enyi wajumbe wenye mbio,

Kwa taifa lenye watu warefu na walio na ngozi laini,*

Kwa watu wanaoogopwa kila mahali,+

Kwa taifa lenye nguvu, linaloshinda,*

Ambalo nchi yake imefagiliwa na mito.”

 3 Enyi wakaaji wote wa nchi nanyi wakaaji wa dunia,

Mtakachoona kitakuwa kama ishara* iliyoinuliwa juu ya milima,

Nanyi mtasikia sauti kama ya pembe inapopigwa.

 4 Kwa maana Yehova aliniambia hivi:

“Nitaendelea kutulia na kutazama* mahali pangu palipofanywa imara,

Kama joto linalometameta pamoja na mwangaza wa jua,

Kama wingu la umande katika joto la mavuno.

 5 Kwa maana kabla ya mavuno,

Ua linapokamilika na kuwa zabibu inayoiva,

Machipukizi yake yatakatwa kwa miundu

Vikonyo vitakatwa na kuondolewa.

 6 Wote wataachwa waliwe na ndege wanaowinda wa milimani

Na wanyama wa duniani.

Ndege wanaowinda watawala wakati wa kiangazi,

Na wanyama wote wa dunia watawala wakati wa mavuno.

 7 Wakati huo zawadi italetwa kwa Yehova wa majeshi,

Kutoka kwa taifa lenye watu warefu na walio na ngozi laini,*

Kutoka kwa watu wanaoogopwa kila mahali,

Kutoka kwa taifa lenye nguvu, linaloshinda,*

Ambalo nchi yake imefagiliwa na mito,

Mpaka mahali pa jina la Yehova wa majeshi, Mlima Sayuni.”+

Tanzanian sign language publications (2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki