Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Isaya 19
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Isaya—Yaliyomo

      • Tangazo dhidi ya Misri (1-15)

      • Wamisri watamjua Yehova (16-25)

        • Madhabahu kwa ajili ya Yehova nchini Misri (19)

Isaya 19:1

Marejeo

  • +Yer 25:17, 19; Eze 29:2; Yoe 3:19
  • +Kut 12:12; Yer 43:12; 46:25; Eze 30:13

Isaya 19:3

Marejeo

  • +Isa 19:11, 13
  • +Isa 8:19; Mdo 16:16; Ufu 18:23

Isaya 19:4

Marejeo

  • +Isa 20:3, 4; Yer 46:25, 26; Eze 29:19

Isaya 19:5

Marejeo

  • +Eze 30:12; Zek 10:11

Isaya 19:6

Marejeo

  • +Kut 2:3

Isaya 19:7

Marejeo

  • +Kum 11:10
  • +Eze 29:10

Isaya 19:9

Marejeo

  • +Kut 9:25, 31; Met 7:16

Isaya 19:10

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “watahuzunika katika nafsi.”

Isaya 19:11

Marejeo

  • +Zb 78:12; Eze 30:14
  • +Isa 44:25

Isaya 19:12

Marejeo

  • +Mwa 41:8; 1Fa 4:30; Mdo 7:22

Isaya 19:13

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Memfisi.”

Marejeo

  • +Yer 46:14; Eze 30:13

Isaya 19:14

Marejeo

  • +Ayu 12:20, 24; Isa 19:3

Isaya 19:15

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “tawi la mtende au tete.”

Isaya 19:16

Marejeo

  • +Isa 11:15

Isaya 19:17

Marejeo

  • +Isa 20:3, 4; Yer 25:17, 19; 43:10, 11; Eze 29:6

Isaya 19:18

Marejeo

  • +Yer 43:4, 7; 44:1

Isaya 19:22

Marejeo

  • +Isa 19:1; Yer 46:13

Isaya 19:23

Marejeo

  • +Isa 11:16; 35:8; 40:3

Isaya 19:24

Marejeo

  • +Zek 2:11

Isaya 19:25

Marejeo

  • +Kum 32:9; Zb 115:12; Isa 61:9

Jumla

Isa. 19:1Yer 25:17, 19; Eze 29:2; Yoe 3:19
Isa. 19:1Kut 12:12; Yer 43:12; 46:25; Eze 30:13
Isa. 19:3Isa 19:11, 13
Isa. 19:3Isa 8:19; Mdo 16:16; Ufu 18:23
Isa. 19:4Isa 20:3, 4; Yer 46:25, 26; Eze 29:19
Isa. 19:5Eze 30:12; Zek 10:11
Isa. 19:6Kut 2:3
Isa. 19:7Kum 11:10
Isa. 19:7Eze 29:10
Isa. 19:9Kut 9:25, 31; Met 7:16
Isa. 19:11Zb 78:12; Eze 30:14
Isa. 19:11Isa 44:25
Isa. 19:12Mwa 41:8; 1Fa 4:30; Mdo 7:22
Isa. 19:13Yer 46:14; Eze 30:13
Isa. 19:14Ayu 12:20, 24; Isa 19:3
Isa. 19:16Isa 11:15
Isa. 19:17Isa 20:3, 4; Yer 25:17, 19; 43:10, 11; Eze 29:6
Isa. 19:18Yer 43:4, 7; 44:1
Isa. 19:22Isa 19:1; Yer 46:13
Isa. 19:23Isa 11:16; 35:8; 40:3
Isa. 19:24Zek 2:11
Isa. 19:25Kum 32:9; Zb 115:12; Isa 61:9
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Isaya 19:1-25

Isaya

19 Tangazo dhidi ya Misri:+

Tazama! Yehova amepanda juu ya wingu linaloenda kwa kasi, naye anakuja Misri.

Miungu ya ubatili ya Misri itatetemeka mbele zake,+

Na moyo wa Misri utayeyuka ndani yake.

 2 “Nitawachochea Wamisri dhidi ya Wamisri,

Nao watapigana,

Kila mmoja atapigana na ndugu yake na jirani yake,

Jiji litapigana na jiji, ufalme utapigana na ufalme.

 3 Na roho ya Misri itakuwa na msukosuko ndani yake,

Nami nitavuruga mipango yake.+

Watatafuta msaada kutoka kwa miungu ya ubatili,

Kwa wachawi na kwa wanaowasiliana na roho na kwa wabashiri.+

 4 Nitaitia Misri mikononi mwa bwana aliye katili,

Na mfalme mkali atawatawala,”+ asema Bwana wa kweli, Yehova wa majeshi.

 5 Na maji ya bahari yatakaushwa,

Na mto utakauka na kuwa mkavu.+

 6 Na mito itanuka;

Mifereji ya Nile ya Misri itapungua na kukauka.

Matete na mafunjo yataoza.+

 7 Mimea iliyo kandokando ya Mto Nile, kwenye kinywa cha Mto Nile,

Na ardhi yote iliyopandwa mbegu kandokando ya Nile+ itakauka.+

Itapeperushwa mbali, nayo haitakuwepo tena.

 8 Na wavuvi wataomboleza,

Wale wanaotupa ndoano ndani ya Mto Nile wataomboleza,

Na wale wanaotandaza nyavu zao juu ya maji watapungua.

 9 Mafundi wa kitani kilichochambuliwa+

Na wafumaji wa vitambaa vyeupe wataaibishwa.

10 Wafumaji wake watapondwa;

Vibarua wote watahuzunika.*

11 Wakuu wa Soani+ ni wapumbavu.

Washauri wenye hekima zaidi wa Farao wanatoa ushauri usio wa busara.+

Mnawezaje kumwambia Farao:

“Mimi ni mzao wa watu wenye hekima,

Mzao wa wafalme wa kale”?

12 Basi, wako wapi watu wenu wenye hekima?+

Acheni wawaambie kama wanajua kile ambacho Yehova wa majeshi ameamua kuhusu Misri.

13 Wakuu wa Soani wametenda kwa upumbavu;

Wakuu wa Nofu*+ wamedanganywa;

Wakuu wa makabila yake wameipotosha Misri.

14 Yehova amemmwagia roho ya mvurugo;+

Nao wameipotosha Misri katika kila jambo inalofanya,

Kama mlevi anavyogaagaa kwenye matapishi yake.

15 Na Misri haitakuwa na kazi yoyote ya kufanya,

Iwe ni kwa ajili ya kichwa au mkia, chipukizi au utete.*

16 Siku hiyo Misri itakuwa kama wanawake, itatetemeka na kuogopa kwa sababu ya mkono wenye kutisha ambao Yehova wa majeshi anainua dhidi yake.+ 17 Na nchi ya Yuda itaifanya Misri iogope. Watahofu kila mara Yuda inapotajwa kwa sababu ya uamuzi ambao Yehova wa majeshi amefanya dhidi yao.+

18 Siku hiyo kutakuwa na majiji matano katika nchi ya Misri yanayozungumza lugha ya Kanaani+ na kuapa kuwa washikamanifu kwa Yehova wa majeshi. Jiji moja litaitwa Jiji la Kubomoa.

19 Siku hiyo kutakuwa na madhabahu kwa ajili ya Yehova katikati ya nchi ya Misri na nguzo kwa ajili ya Yehova kwenye mpaka wake. 20 Itakuwa ishara na ushahidi kwa Yehova wa majeshi nchini Misri; kwa maana watamlilia Yehova kwa sauti kwa sababu ya wakandamizaji, naye atawapelekea mwokozi, aliye mkuu, ambaye atawaokoa. 21 Na Yehova atajulikana kwa Wamisri, na Wamisri watamjua Yehova siku hiyo, nao watatoa dhabihu na zawadi na kuweka nadhiri kwa Yehova na kuitimiza. 22 Yehova ataipiga Misri,+ ataipiga na kuiponya; nao watamrudia Yehova, naye atasikiliza maombi yao ya kusihi na kuwaponya.

23 Siku hiyo kutakuwa na barabara kuu+ kutoka Misri kwenda Ashuru. Kisha Ashuru itakuja Misri, na Misri itaenda Ashuru; na Misri itamtumikia Mungu pamoja na Ashuru. 24 Siku hiyo Israeli itakuwa ya tatu pamoja na Misri na pamoja na Ashuru,+ baraka katikati ya dunia, 25 kwa maana Yehova wa majeshi atakuwa amewabariki, akisema: “Wabarikiwe watu wangu, Misri, na kazi ya mikono yangu, Ashuru, na urithi wangu, Israeli.”+

Tanzanian sign language publications (2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki