-
Mambo ya Walawi 14:49-53Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
49 Ili kuitakasa nyumba hiyo isiyo safi,* atachukua ndege wawili, tawi la mwerezi, kitambaa cha rangi nyekundu, na tawi la hisopo.+ 50 Atamchinjia ndege mmoja kwenye chombo cha udongo chenye maji ya kijito. 51 Kisha atamchukua ndege aliye hai na kumtumbukiza pamoja na tawi la mwerezi, kitambaa cha rangi nyekundu, na tawi la hisopo ndani ya damu ya ndege aliyechinjiwa kwenye maji ya kijito, naye atainyunyiza kuelekea nyumba hiyo mara saba.+ 52 Naye ataitakasa nyumba hiyo isiyo safi* kwa kutumia damu ya ndege huyo, maji ya kijito, yule ndege aliye hai, tawi la mwerezi, tawi la hisopo, na kitambaa cha rangi nyekundu. 53 Kisha atamwachilia ndege aliye hai aende zake mashambani nje ya jiji, naye ataitolea nyumba hiyo dhabihu ya kufunika dhambi, nayo itakuwa safi.
-
-
Hesabu 19:6Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
6 Halafu kuhani atachukua tawi la mwerezi, tawi la hisopo,+ na kitambaa chekundu na kutupa vitu hivyo katika moto unaomteketeza ng’ombe huyo.
-