-
Kumbukumbu la Torati 29:22-24Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
22 “Kizazi cha wakati ujao cha wana wenu na pia wageni kutoka nchi ya mbali watakapoona mapigo ya nchi, magonjwa ambayo Yehova ameleta juu yake— 23 kiberiti na chumvi na kuteketea, hivi kwamba nchi yote haitapandwa wala kuchipuza mimea, wala hakuna mmea wowote utakaoota ndani yake, kama ilivyokuwa wakati wa maangamizi ya Sodoma na Gomora,+ Adma na Seboiimu,+ majiji ambayo Yehova aliyaangamiza katika hasira yake na katika ghadhabu yake— 24 wao pamoja na mataifa yote watauliza, ‘Kwa nini Yehova aliitendea hivi nchi hii?+ Ni nini kilichomfanya awake hasira kali hivi?’
-
-
Yeremia 18:16Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
Kila mtu atakayepita kando yake atatazama kwa mshtuko na kutikisa kichwa chake.+
-
-
Ezekieli 5:15Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
15 Utakuwa kitu cha kushutumiwa na kudharauliwa,+ mfano wa kuonya na tisho kwa mataifa yanayokuzunguka, nitakapotekeleza hukumu dhidi yako kwa hasira na ghadhabu na kwa adhabu kali. Mimi, Yehova, nimesema.
-