-
Marko 6:17-20Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
17 Kwa maana Herode alikuwa ameagiza Yohana akamatwe na kufungwa gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo ndugu yake. Kwa sababu Herode alikuwa amemwoa.+ 18 Kwa maana Yohana alikuwa akimwambia Herode: “Si halali kwako kuwa na mke wa ndugu yako.”+ 19 Basi Herodia alikuwa na kinyongo kumwelekea Yohana na alitaka kumuua, lakini hakuweza. 20 Kwa maana Herode alimwogopa Yohana kwa kuwa alijua ni mtu mwadilifu na mtakatifu,+ naye alikuwa akimlinda. Baada ya kumsikiliza, hakujua la kufanya, lakini bado aliendelea kumsikiliza kwa furaha.
-