-
1 Samweli 21:1-6Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
21 Baadaye Daudi akafika Nobu+ kwa kuhani Ahimeleki. Ahimeleki alianza kutetemeka alipokutana na Daudi, akamuuliza: “Kwa nini uko peke yako na hujaja na mtu yeyote?”+ 2 Daudi akamjibu kuhani Ahimeleki: “Mfalme aliniagiza nifanye jambo fulani, lakini akaniambia, ‘Usimjulishe mtu yeyote kazi niliyokutuma kufanya na maagizo niliyokupa.’ Nilikubaliana na vijana wangu tukutane mahali fulani. 3 Sasa ikiwa una mikate mitano, nipe tu, au chochote kinachopatikana.” 4 Lakini kuhani akamwambia Daudi: “Kwa sasa hakuna mikate ya kawaida, lakini kuna mikate mitakatifu+—ninaweza kukupa tu ikiwa vijana wako wamejiepusha na wanawake.”*+ 5 Daudi akamwambia hivi kuhani: “Kwa hakika tumejitenga kabisa na wanawake kama tulivyofanya awali nilipoenda vitani.+ Ikiwa miili ya vijana hawa ni mitakatifu hata katika shughuli za kawaida, je, si mitakatifu zaidi leo?” 6 Basi kuhani akampa mikate mitakatifu,+ kwa sababu hakukuwa na mikate mingine isipokuwa mikate ya wonyesho iliyokuwa imeondolewa mbele za Yehova na mikate mipya kuwekwa siku hiyo.
-