Zaburi
147 Msifuni Yah!*
3 Huwaponya waliovunjika moyo;
Huyafunga majeraha yao.
4 Huhesabu idadi ya nyota;
Zote anaziita kwa majina.+
6 Yehova huwainua wapole,+
Lakini huwatupa chini waovu.
7 Mwimbieni Yehova kwa shukrani;
Mwimbieni sifa Mungu wetu kwa kinubi,
8 Yeye anayezifunika mbingu kwa mawingu,
Yeye anayeiletea dunia mvua,+
Yeye anayechipusha majani+ milimani.
12 Mtukuze Yehova, Ee Yerusalemu.
Msifu Mungu wako, Ee Sayuni.
13 Huyafanya makomeo ya malango ya jiji lako yawe imara;
Huwabariki wana wako walio ndani yako.
15 Huituma amri yake duniani;
Neno lake hukimbia upesi sana.
17 Huyatupa chini mawe yake ya mvua* kama chembe za mkate.+
Ni nani anayeweza kustahimili baridi yake?+
18 Hulituma neno lake, nayo inayeyuka.
Huufanya upepo wake uvume,+ maji yanatiririka.
19 Anamtangazia Yakobo neno lake,
Na Israeli masharti yake na hukumu zake.+
20 Hajalifanyia hivyo taifa lingine lolote;+
Hawajui lolote kuhusu hukumu zake.