WIMBO NA. 10
Msifuni Yehova Mungu Wetu!
- 1. Sifu Yah, Yehova Mungu! - Tangazeni jina lake! - Tangaza mwisho karibu, - Wote wasikie ujumbe. - Yehova Mungu ameagiza - Kwamba sasa ni wakati - Mwanaye atawale, - Tangaza baraka zake zijazo! - (KORASI) - Sifu Yah, Yehova Mungu! - Tangazeni fahari yake! 
- 2. Sifu Yah, na kumwimbia! - Lisifuni jina lake! - Kwa shangwe, toka moyoni, - Utukufu wake tangaza. - Mungu ni mwema kwa watu wote, - Licha ya fahari yake. - Anajua mahitaji yetu, - Huitika tumwitapo. - (KORASI) - Sifu Yah, Yehova Mungu! - Tangazeni fahari yake! 
(Ona pia Zab. 89:27; 105:1; Yer. 33:11.)