WIMBO NA. 159
Mpe Yehova Utukufu
- 1. Mwenye enzi, Ee Yehova, - Ukiwa ju’ mbinguni. - Naweza kukupa nini - Kwa upendo wako mwingi? - Nitazamapo angani, - Naona nguvu zako. - Mimi ni nani Yehova, - Unipe kibali chako? - (KORASI) - Ee Yehova, ninakuimbia. - Wimbo wa kukusifu. - Mungu wangu, mfalme milele, - Unastahili sifa; - Utukufu ni wako. 
- 2. Maisha yangu nakupa. - Nitakusifu wewe. - Kutangaza njia zako - Na kusema wema wako. - Najivunia Yehova, - Kukuabudu wewe. - Wanipa nguvu na shangwe, - Uniongoze milele. - (KORASI) - Ee Yehova, ninakuimbia. - Wimbo wa kukusifu. - Mungu wangu, mfalme milele, - Unastahili sifa; - Utukufu ni wako. 
- 3. Mabonde mito bahari, - Jua mwezi na nyota - Hunista’jabisha mimi - Upendo bila kifani. - Hekima na utukufu: - Naona mambo hayo. - Kwa nini nisikusifu - Kwa vyote ulivyoumba? - (KORASI) - Ee Yehova, ninakuimbia. - Wimbo wa kukusifu. - Mungu wangu, mfalme milele, - Unastahili sifa; - Utukufu ni wako. 
(Ona pia Zb. 96:1-10; 148:3, 7.)