WIMBO NA. 13
Kristo, Kielelezo Chetu
- 1. Yehova ni mwenye, - upendo na mwema, - Katoa Mwana wake wa Pekee - Awe mwanadamu, - kusudi tumwige - Tulitukuze jina la Mungu 
- 2. Neno la Yehova, - lilimwimarisha. - Kwake lilikuwa kama chakula. - Kawa na hekima, - ufahamu pia, - Katuachia kielelezo 
- 3. Kama Yesu Kristo, - tumsifu Mungu - Tuzifuate hatua za Yesu. - Tumwige daima, - maishani mwetu. - Tutapata kibali cha Mungu. 
(Ona pia Yoh. 8:29; Efe. 5:2; Flp. 2:5-7.)