WIMBO NA 76
Unahisije?
- 1. We‘ unahisije - kuhusu kuhubiri? - Kuwafundisha watu - wanaopendezwa? - Ujitahidipo - Kutimiza huduma - Na Yehova afanye - kazi ya kukuza. - (KORASI) - Tuna shangwe, twafurahi - kujitoa kikamili. - Basi tumsifu Mungu. - Daima dawamu. 
- 2. We‘ unahisije - wanaposikiliza? - Wanapoitikia - ujumbe wa kweli? - Hata wakatae - bado twautangaza. - Twafurahi kuitwa kwa - jina la Mungu. - (KORASI) - Tuna shangwe, twafurahi - kujitoa kikamili. - Basi tumsifu Mungu. - Daima dawamu. 
- 3. We‘ unahisije - kuwa na pendeleo, - Alilotupa Mungu - la kumwakilisha? - Tunajivunia - kutangaza Ufalme - Kuwatafuta watu - wanaostahili. - (KORASI) - Tuna shangwe, twafurahi - kujitoa kikamili. - Basi tumsifu Mungu. - Daima dawamu. 
(Ona pia Mdo. 13:48; 1 The. 2:4; 1 Tim. 1:11.)