Programu Ya Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi Ya 1999
MAAGIZO
Katika 1999, Shule ya Huduma ya Kitheokrasi itaendeshwa kama ifuatavyo.
VITABU: Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo [bi7-SW], Mnara wa Mlinzi [w-SW], Amkeni! [g-SW], “Kila Andiko Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa” (Chapa ya 1990) [si-SW], Siri ya Kupata Furaha ya Familia [fy-SW], na Étude perspicace des Écritures [it-2-F] au Auxiliaire pour une meilleure intelligence de la Bible [ad].
Shule inapaswa kuanza PA WAKATI kwa wimbo na sala. Baada ya maneno ya utangulizi, shule itaendeshwa kama ifuatavyo:
KIPINDI Na. 1: Dakika 15. Hotuba hii ingepaswa kutolewa na mzee au mtumishi wa huduma, na itakuwa na msingi juu ya Mnara wa Mlinzi, Amkeni!, au “Kila Andiko Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa.” Inapokuwa na msingi juu ya Mnara wa Mlinzi au Amkeni!, itatolewa kama vile hotuba ya maagizo ya dakika 15 bila kujikumbusha kwa mdomo; inapokuwa na msingi juu ya kitabu “Kila Andiko,” Itatolewa kama vile hotuba ya maagizo ya dakika 10 hadi 12 ikifuatwa na kujikumbusha kwa mdomo kwa dakika 3 hadi 5 kwa kutumia maulizo yaliyochapwa katika kichapo. Lengo halipaswi kuwa tu kutoa habari hiyo bali pia kuvuta fikira kwenye manufaa ya habari inayozungumziwa na kukazia yale yatakayokuwa yenye kusaidia zaidi kutaniko. Kichwa kinachoonyeshwa chapaswa kutumiwa.
Ndugu wanaopewa hotuba hii wanapaswa kuwa waangalifu ili kuheshimu wakati uliowekwa. Ikiwa wanatolewa shauri la faragha, maandishi yanayopatana na jambo hilo yapaswa kufanywa juu ya karatasi zao za shauri.
MAMBO MAKUU KUTOKANA NA USOMAJI WA BIBLIA: Dakika 6. Sehemu hii itatolewa na mzee au mtumishi wa huduma atakayeonyesha kwa matokeo jinsi habari hiyo inavyohusu mahitaji ya kutaniko. Haipaswi kuwa tu muhtasari (kifupi) wa usomaji aliogawiwa. Mawazo makuu ya sura alizogawiwa yanaweza kutiwa ndani kwa sekunde 30 hadi 60 tu. Hata hivyo, lengo kuu ni kusaidia wasikilizaji wafahamu ni kwa nini na jinsi gani habari hiyo ni yenye manufaa kwetu. Kisha sehemu hii, mwangalizi wa shule ataomba wanafunzi kwenda katika madarasa yao mbalimbali.
KIPINDI Na. 2: Dakika 5. Huu ni usomaji wa Biblia utakaofanywa na ndugu. Mpango huu unatumika katika shule kubwa na pia katika vikundi vidogo vya shule. Kwa kawaida, migawo ya kusoma ni mifupi vya kutosha ili kuruhusu mwanafunzi atoe maelezo mafupi ya utangulizi na ya kumalizia. Habari za kihistoria, maana ya unabii au ya mafundisho na pia matumizi ya kanuni vyaweza kutiwa ndani. Mistari yote iliyotolewa kuwa mgawo yapasa isomwe bila kukatizwa. Bila shaka, ikiwa mistari inayopasa isomwe haifuatani mfululizo, mwanafunzi anaweza kutaja mstari ambapo usomaji waendelea.
KIPINDI Na. 3: Dakika 5. Kipindi hiki kitatolewa kwa dada. Habari ya kuzungumziwa itakuwa na msingi juu ya vitabu Siri ya Kupata Furaha ya Familia, Étude perspicace des Écritures au Auxiliaire pour une meilleure intelligence de la Bible. (Ona kipindi Na. 4 kwa ajili ya maelezo kuhusu jinsi ya kutoa habari juu ya watu wa kibiblia.) Kikao chaweza kuwa ushahidi wa vivi hivi, ziara ya kurudia, funzo la Biblia la nyumbani, au upande fulani mwingine wa utumishi wa shambani. Wakati mwingine, inawezekana kutia ndani mzazi mwenye kushiriki habari pamoja na mtoto mwenye umri mdogo. Washiriki wa kipindi hicho wanaweza kuketi au kusimama. Mwangalizi wa shule atapenda hasa kuona jinsi mwanafunzi anavyomsaidia msikilizaji au mtoto afikiri juu ya habari na aelewe jinsi maandiko yanavyotumiwa. Mwanafunzi anayepewa sehemu hii anapaswa kujua kusoma. Mwenzi mmoja wa kike atachaguliwa na mwangalizi wa shule, lakini mwenzi mwingine wa pili anaweza kushiriki katika kipindi. Mwanafunzi ataamua ikiwa msikilizaji atasoma baadhi ya mafungu watakapokuwa wenye kuchunguza kitabu Furaha ya Familia. Uangalifu mwingi wapaswa kutolewa juu ya namna nzuri ya kutumikisha mawazo, si juu ya kikao.
KIPINDI Na. 4: Dakika 5. Kinapokuwa na msingi juu ya mtu wa kibiblia, kipindi hiki kitatolewa kwa ndugu au dada. Kinapokuwa na msingi juu ya kitabu Furaha ya Familia, kitatolewa kwa ndugu. Kwa kila kipindi, kichwa kinaonyeshwa katika programu. Kipindi hiki kinapokuwa na msingi juu ya mtu fulani wa kibiblia, habari inaweza kupatikana katika kitabu Étude perspicace des Écritures au Auxiliaire pour une meilleure intelligence de la Bible, chini ya jina lake. Mwanafunzi anapaswa kujifunza mitajo ya Maandiko katika habari kusudi apate mwono ulio wazi wa mtu huyo wa kibiblia—matukio ya maisha yake, na vilevile utu wake, tabia zake, na msimamo wake. Baadaye, mwanafunzi atazungumzia kichwa cha habari alichogawiwa kwa msaada wa maandiko yaliyochaguliwa kwa makini. Ataweza pia kuingiza maandiko mengine yanayokazia kanuni za kibiblia zinazoambatana na kichwa. Kusudi la kufikiria mtu wa kibiblia ni kuonyesha yale ambayo tunaweza kujifunza kutokana na kielelezo chake. Matendo ya uaminifu, uhodari, unyenyekevu na kutokuwa mwenye ubinafsi ni vielelezo vyema vya kufuatwa; matendo ya kukosa uaminifu na vitabia vya utu visivyopendeza vinaweza kuwa maonyo juu ya mwenendo ambao Wakristo wanapaswa kutupilia mbali. Ikiwa ndugu ndiye anayepewa kipindi hiki, yeye angepaswa kukitoa akifikiria wasikilizaji wote wa Jumba la Ufalme. Ikiwa ni dada anayetoa kipindi hiki, atafuata mashauri yanayotolewa kwa ajili ya kipindi Na. 3.
*PROGRAMU YA ZIADA YA USOMAJI WA BIBLIA: Inapatikana kati ya vifungu vya mraba [] baada ya namba ya wimbo wa juma. Kwa kufuata programu hii ya usomaji wa kurasa zapata kumi kwa juma, inawezekana kusoma Biblia yote nzima kwa muda wa miaka mitatu. Hakuna sehemu yoyote ya shule au ya kujikumbusha kwa kuandika inayokuwa na msingi juu ya programu hiyo ya ziada ya usomaji.
TAARIFA: Kwa ajili ya maelezo zaidi juu ya mashauri, wakati, kujikumbusha kwa kuandika na kutayarisha vipindi, tafadhali angalieni ukurasa 3 wa Huduma Yetu ya Ufalme ya Novemba 1996.
PROGRAMU
Januari 4 Usomaji wa Biblia: Ufunuo 16-18
Wimbo Na. 23 [*2 Wafalme 16-19]
Na. 1: Jinsi Mungu Alivyopulizia Biblia (w97-SW 6/15 kur. 4-8)
Na. 2: Ufunuo 16:1-16
Na. 3: Mlinde Mtoto Wako Dhidi ya Madhara (fy-SW kur. 61-3 maf. 24-8)
Na. 4: Mathayo (Matthieu)—Kichwa: Mungu Hana Upendeleo
Januari 11 Usomaji wa Biblia: Ufunuo 19-22
Wimbo Na. 126 [*2 Wafalme 20-25]
Na. 1: Ufunuo—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 268-9 maf. 28-34)
Na. 2: Ufunuo 22:1-15
Na. 3: Wazazi—Fanyeni Uwasiliano Uweko Sikuzote (fy-SW kur. 64-6 maf. 1-7)
Na. 4: Mathiasi—Kichwa: Mungu Anataka Kwamba Waangalizi Wawe Wanaume wa Kiroho
Januari 18 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 1-3
Wimbo Na. 84 [*1 Mambo ya Siku 1-6]
Na. 1: Mwanzo: Utangulizi (si-SW kur. 13-14 maf. 1-8)
Na. 2: Mwanzo 1:1-13
Na. 3: Fundisheni Watoto Kanuni za Kiadili na za Kiroho (fy-SW kur. 67-70 maf. 8-14)
Na. 4: Melkizedeki (Melkisédec)—Kichwa: Yesu Kristo, Kuhani Mkuu Kulingana na Namna ya Melkizedeki
Januari 25 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 4-6
Wimbo Na. 66 [*1 Mambo ya Siku 7-13]
Na. 1: Jihadhari na Kuhesabia Wengine Nia Mbaya (w97-SW 5/15 kur. 26-9)
Na. 2: Mwanzo 4:1-16
Na. 3: Kwa Nini Nidhamu na Staha Ni vya Lazima (fy-SW kur. 71-2 maf. 15-18)
Na. 4: Mefiboshethi (Mephibosheth) (Na. 2)—Kichwa: Fadhili Zenye Upendo—Alama ya Watumishi wa Kweli wa Mungu
Februari 1 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 7-9
Wimbo Na. 108 [*1 Mambo ya Siku 14-21]
Na. 1: Habari ya Biblia Kuhusu Gharika Ni ya Kweli (g97-SW 2/8 kur. 26-7)
Na. 2: Mwanzo 7:1-16
Na. 3: Fundisheni Watoto Maoni ya Mungu juu ya Kazi na Kucheza (fy-SW kur. 72-5 maf. 19-25)
Na. 4: Meshaki—Kichwa: Kushika Uaminifu-Maadili Katika Ujana Huleta Thawabu
Februari 8 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 10-12
Wimbo Na. 132 [*1 Mambo ya Siku 22-29]
Na. 1: Kweli Kuhusu Uongo (g97-SW 2/22 kur. 17-19)
Na. 2: Mwanzo 12:1-20
Na. 3: Uasi wa Watoto na Sababu Zake (fy-SW kur. 76-9 maf. 1-8)
Na. 4: Mika (Mika) (Na. 8 it-2-F au Na. 2 ad)—Kichwa: Nguvu za Vielezi
Februari 15 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 13-15
Wimbo Na. 49 [*2 Mambo ya Siku 1-8]
Na. 1: Udhaifu wa Kibinadamu Hutukuza Nguvu za Yehova (w97-SW 6/1 kur. 24-7)
Na. 2: Mwanzo 14:8-20
Na. 3: Mikaya (Micaïah) (Na. 2 it-2-F) Kichwa: Hubiri kwa Uhodari
Na. 4: Usiwe Mwenye Uendekevu Wala Mwenye Uzuifu Kupita Kiasi (fy-SW kur. 80-2 maf. 10-13)
Februari 22 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 16-19
Wimbo Na. 188 [*2 Mambo ya Siku 9-17]
Na. 1: Kinachofunuliwa na Sala Zako (w97-SW 7/1 kur. 27-30)
Na. 2: Mwanzo 18:1-15
Na. 3: Kutimiza Mahitaji ya Msingi ya Mtoto Kwaweza Kuzuia Uasi (fy-SW kur. 82-5 maf. 14-18)
Na. 4: Miriamu (Miriam) (Na. 1 it-2-F)—Kichwa: Jihadhari na Kunung’unika
Machi 1 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 20-23
Wimbo Na. 54 [*2 Mambo ya Siku 18-24]
Na. 1: Jinsi ya Kuizoeza Dhamiri Yako (w97-SW 8/1 kur. 4-6)
Na. 2: Mwanzo 23:1-13
Na. 3: Mordekai (Mordekaï) (Na. 2 it-2-F)—Kichwa: Uaminifu, Sifa Yenye Kuthawabisha
Na. 4: Njia za Kusaidia Mtoto Anayefanya Kosa (fy-SW kur. 85-7 maf. 19-23)
Machi 8 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 24-25
Wimbo Na. 121 [*2 Mambo ya Siku 25-31]
Na. 1: Kweli Huweka Huru Kutoka Mambo Gani? (w97-SW 2/1 kur. 4-7)
Na. 2: Mwanzo 24:1-4, 10-21
Na. 3: Musa (Moïse)—Kichwa: Tuthamini Kuzoezwa na Yehova
Na. 4: Kumshughulikia Mwasi Aliyeazimia (fy-SW kur. 87-9 maf. 24-7)
Machi 15 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 26-28
Wimbo Na. 197 [*2 Mambo ya Siku 32-36]
Na. 1: Mahali pa Muziki Katika Ibada ya Kisasa (w97-SW 2/1 kur. 24-8)
Na. 2: Mwanzo 26:1-14
Na. 3: Ilinde Familia Yako Dhidi ya Mavutano Yaletayo Uharibifu (fy-SW kur. 90-2 maf. 1-7)
Na. 4: Naamani (Naamân) (Na. 2 it-2-F)—Kichwa: Unyenyekevu Huvuna Baraka Tele
Machi 22 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 29-31
Wimbo Na. 4 [*Ezra 1-7]
Na. 1: Dunia Haitakwisha Katika Moto (g97-SW 1/8 kur. 26-7)
Na. 2: Mwanzo 31:1-18
Na. 3: Nabali (Nabal)—Kichwa: Tusilipe Mabaya kwa Mema
Na. 4: Maoni ya Mungu juu ya Ngono (fy-SW kur. 92-4 maf. 8-13)
Machi 29 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 32-35
Wimbo Na. 143 [*Ezra 8–Nehemia 4]
Na. 1: Maponyo ya Kimuujiza Kutoka kwa Mungu—Wakati Gani? (w97-SW 7/1 kur. 4-7)
Na. 2: Mwanzo 35:1-15
Na. 3: Saidia Watoto Wako Wachague Marafiki Wazuri (fy-SW kur. 95-7 maf. 14-18)
Na. 4: Nadabu (Nadab) (Na. 1)—Kichwa: Kutumia Vibaya Mapendeleo Hutokeza Kutokubaliwa na Yehova
Aprili 5 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 36-38
Wimbo Na. 106 [*Nehemia 5-11]
Na. 1: Wokovu—Unachomaanisha kwa Kweli (w97-SW 8/15 kur. 4-7)
Na. 2: Mwanzo 38:6-19, 24-26
Na. 3: Nathani (Nathân) (Na. 2 it-2-F au Na. 1 ad)—Kichwa: Tusijizuie Kurekebisha Yeyote Anayehitaji Hivyo
Na. 4: Kuchagua Tafrija Yenye Kufaa ya Familia (fy-SW kur. 97-102 maf. 19-27)
Aprili 12 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 39-41
Wimbo Na. 34 [*Nehemia 12–Esiteri 5]
Na. 1: Kwa Nini Lililo Baya Liripotiwe? (w97-SW 8/15 kur. 26-9)
Na. 2: Mwanzo 40:1-15
Na. 3: Ujuzi wa Kimaandiko kwa Ajili ya Familia ya Mzazi Mmoja. (fy-SW kur. 103-5 maf. 1-8)
Na. 4: Nathanaeli (Nathanaël)—Kichwa: Epuka Kuwa Mwenye Hila
Aprili 19 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 42-44
Wimbo Na. 124 [*Esiteri 6–Yobu 5]
Na. 1: Kwa Nini Udhibiti Hasira Yako (g97-SW 6/8 kur. 18-19)
Na. 2: Mwanzo 42:1-17
Na. 3: Ugumu wa Kupata Riziki Mtu Akiwa Mzazi Pekee (fy-SW kur. 105-7 maf. 9-12)
Na. 4: Nebukadneza (Neboukadnetsar)—Kichwa: Yehova Hushusha Wale Wanaotembea kwa Kiburi
Aprili 26 Kujikumbusha kwa Kuandika. Malizeni Ufunuo 16—Mwanzo 44
Wimbo Na. 18 [*Yobu 6-14]
Mei 3 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 45-47
Wimbo Na. 90 [*Yobu 15-23]
Na. 1: Je! Misherehekeo ya Mavuno Humpendeza Mungu? (w97-SW 9/15 kur. 8-9)
Na. 2: Mwanzo 45:16–46:4
Na. 3: Kudumisha Nidhamu Katika Nyumba ya Mzazi Mmoja (fy-SW kur. 108-10 maf. 13-17)
Na. 4: Nebuzaradani (Nebouzaradân)—Kichwa: Neno la Yehova Halishindwi Kamwe
Mei 10 Usomaji wa Biblia: Mwanzo 48-50
Wimbo Na. 76 [*Yobu 24-33]
Na. 1: Mwanzo—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 17-19 maf. 30-5)
Na. 2: Mwanzo 49:13-28
Na. 3: Kushinda Vita Dhidi ya Upweke (fy-SW kur. 110-13 maf. 18-22)
Na. 4: Nehemia (Nehémia) (Na. 3 it-2-F)—Kichwa: Iweni Vielelezo kwa Kundi
Mei 17 Usomaji wa Biblia: Kutoka 1-4
Wimbo Na. 2 [*Yobu 34-42]
Na. 1: Kutoka: Utangulizi (si-SW kur. 19-20 maf. 1-8)
Na. 2: Kutoka 4:1-17
Na. 3: Nikodemo (Nicodème)—Kichwa: Kuwaogopa Wanadamu Huleta Mtego
Na. 4: Jinsi ya Kusaidia Familia za Mzazi Mmoja (fy-SW kur. 113-15 maf. 23-7)
Mei 24 Usomaji wa Biblia: Kutoka 5-8
Wimbo Na. 42 [*Zaburi 1-17]
Na. 1: Tariji Ingawa Maskini—Yawezekanaje? (w97-SW 9/15 kur. 3-7)
Na. 2: Kutoka 7:1-13
Na. 3: Noa (Noé)—Kichwa: Utii Ni wa Lazima kwa Ajili ya Uhai
Na. 4: Faida za Kukabiliana na Ugonjwa Ukiwa na Maoni ya Kimungu (fy-SW kur. 116-19 maf. 1-9)
Mei 31 Usomaji wa Biblia: Kutoka 9-12
Wimbo Na. 24 [*Zaburi 18-28]
Na. 1: Maana ya kutokuwa Sehemu ya Ulimwengu (g97-SW 9/8 kur. 12-13)
Na. 2: Kutoka 12:21-36
Na. 3: Ubora wa Roho Yenye Kuponya (fy-SW kur. 120-1 maf. 10-13)
Na. 4: Obadia (Obadia) (Na. 4 it-2-F au Na. 1 ad)—Kichwa: Onyesha Upendo kwa Watu wa Mungu na Usiwe Mwenye Hofu
Juni 7 Usomaji wa Biblia: Kutoka 13-16
Wimbo Na. 58 [*Zaburi 29-38]
Na. 1: Jinsi ya Kupata Tumaini Katikati ya Hali ya Kukata Tumaini (w97-SW 5/15 kur. 22-5)
Na. 2: Kutoka 15:1-13
Na. 3: Weka Mambo ya Kutangulizwa na Saidia Watoto Wakabiliane na Ugonjwa Katika Familia (fy-SW kur. 122-3 maf. 14-18)
Na. 4: Onesimo (Onésime)—Kichwa: Shikilia Dhamiri Safi
Juni 14 Usomaji wa Biblia: Kutoka 17-20
Wimbo Na. 115 [*Zaburi 39-50]
Na. 1: Jinsi Wakristo Wanavyowaheshimu Wazazi Wazee-Wazee (w97-SW 9/1 kur. 4-7)
Na. 2: Kutoka 17:1-13
Na. 3: Paulo (Paul)—Kichwa: Maadui wa Kweli Waweza Kubadilika
Na. 4: Jinsi ya Kuona Matibabu (fy-SW kur. 124-6 maf. 19-23)
Juni 21 Usomaji wa Biblia: Kutoka 21-24
Wimbo Na. 5 [*Zaburi 51-65]
Na. 1: Sayansi ya Kweli Hupatana na Biblia no ref. (g97-SW 7/8 kur. 26-7)
Na. 2: Kutoka 21:1-15
Na. 3: Mke Anayeamini Awezaje Kudumisha Amani Katika Nyumba Yenye Kugawanyika? (fy-SW kur. 128-32 maf. 1-9)
Na. 4: Petro (Pierre)—Kichwa: Tuwe Wenye Uhodari na Wenye Bidii kwa Ajili ya Ibada ya Kweli
Juni 28 Usomaji wa Biblia: Kutoka 25-28
Wimbo Na. 47 [*Zaburi 66-74]
Na. 1: Mjue Yehova, Yule Mungu Mwenye Utu (w97-SW 10/1 kur. 4-8)
Na. 2: Kutoka 25:17-30
Na. 3: Filipo (Philipe) (Na. 1)—Kichwa: Tuwe Wenye Busara na Wenye Akili
Na. 4: Mume Anayeamini Anawezaje Kudumisha Amani Katika Nyumba Yenye kugawanyika? (fy-SW kur. 132-3 maf. 10-11)
Julai 5 Usomaji wa Biblia: Kutoka 29-32
Wimbo Na. 174 [*Zaburi 75-85]
Na. 1: Usiruhusu Roho ya Ulimwengu Ikutie Sumu (w97-SW 10/1 kur. 25-9)
Na. 2: Kutoka 29:1-14
Na. 3: Kuwazoeza Watoto Kimaandiko Katika Nyumba Iliyogawanyika (fy-SW kur. 133-4 maf. 12-15)
Na. 4: Filipo (Philipe) (Na. 2)—Kichwa: Tuwe Watu wa Kiroho
Julai 12 Usomaji wa Biblia: Kutoka 33-36
Wimbo Na. 214 [*Zaburi 86-97]
Na. 1: Uwe Mwenye Kutumainika na Ushike Uaminifu-Maadili Wako (w97-SW 5/1 kur. 4-7)
Na. 2: Kutoka 34:17-28
Na. 3: Kudumisha Uhusiano wa Amani Pamoja na Wazazi Walio na Dini Tofauti na Yako (fy-SW kur. 134-5 maf. 16-19)
Na. 4: Finehasi (Phinéas) (Na. 1)—Kichwa: Tuwe Hodari kwa Ajili ya Yale Yaliyo Sawa
Julai 19 Usomaji wa Biblia: Kutoka 37-40
Wimbo Na. 38 [*Zaburi 98-106]
Na. 1: Kutoka—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 24-5 maf. 26-31)
Na. 2: Kutoka 40:1-16
Na. 3: Ugumu wa Kuwa Mzazi wa Kambo (fy-SW kur. 136-9 maf. 20-5)
Na. 4: Finehasi (Phinéas) (Na. 2)—Kichwa: Tusimtendee Yehova Kamwe Mambo ya Kukosa Heshima
Julai 26 Usomaji wa Biblia: Walawi 1-4
Wimbo Na. 26 [*Zaburi 107-118]
Na. 1: Walawi: Utangulizi (si-SW kur. 25-6 maf. 1-10)
Na. 2: Walawi 2:1-13
Na. 3: Usiruhusu Vifuatio vya Kimwili Vigawanye Nyumba Yako (fy-SW kur. 140-1 maf. 26-8)
Na. 4: Fibi (Phœbé)—Kichwa: Tutetee Ndugu Zetu kwa Ujasiri
Agosti 2 Usomaji wa Biblia: Walawi 5-7
Wimbo Na. 9 [*Zaburi 119-125]
Na. 1: Ufunguo wa Furaha Halisi (w97-SW 10/15 kur. 5-7)
Na. 2: Walawi 6:1-13
Na. 3: Matokeo Yenye Kudhuru ya Uraibu wa Alkoholi (fy-SW kur. 142-3 maf. 1-4)
Na. 4: Pilato (Pilate)—Kichwa: Kushindwa na Umati Humfanya Mtu Achukue Lawama
Agosti 9 Usomaji wa Biblia: Walawi 8-10
Wimbo Na. 210 [*Zaburi 126-143]
Na. 1: Kufahamu Kanuni Hudhihirisha Ukomavu (w97-SW 10/15 kur. 28-30)
Na. 2: Walawi 10:12-20
Na. 3: Kusaidia Mshiriki wa Familia Aliye Mraibu wa Alkoholi (fy-SW kur. 143-7 maf. 5-13)
Na. 4: Rabshake (Rabshaqé)—Kichwa: Mungu Hazihakiwi
Agosti 16 Usomaji wa Biblia: Walawi 11-13
Wimbo Na. 80 [*Zaburi 144–Mezali 5]
Na. 1: Jihadhari na “Waepikurea” (w97-SW 11/1 kur. 23-5)
Na. 2: Walawi 13:1-17
Na. 3: Ujeuri wa Kinyumbani na Njia za Kuuepuka (fy-SW kur. 147-9 maf. 14-22)
Na. 4: Raheli (Rachel)—Kichwa: Tukubali Magumu ya Maisha Bila Wivu Wala Kukata Tamaa
Agosti 23 Usomaji wa Biblia: Walawi 14-15
Wimbo Na. 137 [*Mezali 6-14]
Na. 1: Hizi Kwelikweli Ndizo Ziku za Mwisho (w97-SW 4/1 kur. 4-8)
Na. 2: Walawi 14:33-47
Na. 3: Rahabu (Rahab)—Kichwa: Imani Bila Kazi Imekufa
Na. 4: Je! Kutengana Ndilo Suluhisho? (fy-SW kur. 150-2 maf. 23-6)
Agosti 30 Kujikumbusha kwa Kuandika. Malizeni Mwanzo 45–Walawi 15
Wimbo Na. 145 [*Mezali 15-22]
Septemba 6 Usomaji wa Biblia: Walawi 16-18
Wimbo Na. 222 [*Mezali 23-31]
Na. 1: Kuteseka Kutakapokuwa Hakupo Tena (w97-SW 2/15 kur. 4-7)
Na. 2: Walawi 16:20-31
Na. 3: Rebeka (Rébecca)—Kichwa: Fanya Yehova Awe Mwenye Kuhusika Unapochagua Mwenzi
Na. 4: Njia ya Kimaandiko ya Kusuluhisha Matatizo ya Ndoa (fy-SW kur. 153-6 maf. 1-9)
Septemba 13 Usomaji wa Biblia: Walawi 19-21
Wimbo Na. 122 [*Muhubiri 1-12]
Na. 1: Kwa Nini Kujinyima Raha Sio Ufunguo wa Hekima no ref. (g97-SW 10/8 kur. 20-1)
Na. 2: Walawi 19:16-18, 26-37
Na. 3: Rehoboamu (Rehabam)—Kichwa: Tupilia Mbali Kiburi na Mashauri Mabaya
Na. 4: Kutoa Haki ya Ndoa (fy-SW kur. 156-8 maf. 10-13)
Septemba 20 Usomaji wa Biblia: Walawi 22-24
Wimbo Na. 8 [*Wimbo wa Solomoni 1–Isaya 5]
Na. 1: Je! Kulalamika kwa Namna Zote Ni Kubaya? (w97-SW 12/1 kur. 29-31)
Na. 2: Walawi 23:15-25
Na. 3: Rubeni (Ruben) (Na. 1)—Kichwa: Matendo Mabaya Yaweza Kuwa na Matokeo Yenye Kudumu
Na. 4: Misingi ya Kibiblia ya Talaka (fy-SW kur. 158-9 maf. 14-16)
Septemba 27 Usomaji wa Biblia: Walawi 25-27
Wimbo Na. 120 [*Isaya 6-14]
Na. 1: Walawi—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW kur. 28-30 maf. 28-39)
Na. 2: Walawi 25:13-28
Na. 3: Ruthi (Ruth)—Kichwa: Upendo wa Kweli Ni Mwaminifu
Na. 4: Yale Ambayo Maandiko Husema juu ya Kutengana (fy-SW kur. 159-62 maf. 17-22)
Oktoba 4 Usomaji wa Biblia: Hesabu 1-3
Wimbo Na. 30 [*Isaya 15-25]
Na. 1: Hesabu: Utangulizi (si-SW kur. 30-1 maf. 1-10)
Na. 2: Hesabu 1:44-54
Na. 3: Kuzeeka Mkiwa Pamoja (fy-SW kur. 163-5 maf. 1-9)
Na. 4: Salome (Salomé) (Na. 1)—Kichwa: Mtumikie Yehova Ukiwa Mwenye Kiasi
Oktoba 11 Usomaji wa Biblia: Hesabu 4-6
Wimbo Na. 97 [*Isaya 26-33]
Na. 1: Yehova Hutawala kwa Huruma (w97-SW 12/15 kur. 28-9)
Na. 2: Hesabu 4:17-33
Na. 3: Kuimarisha Tena Kifungo Chenu cha Ndoa (fy-SW kur. 166-7 maf. 10-13)
Na. 4: Samsoni (Samson)—Kichwa: Hifadhi Uhusiano Wako Wenye Thamani Pamoja na Yehova
Oktoba 18 Usomaji wa Biblia: Hesabu 7-9
Wimbo Na. 96 [*Isaya 34-41]
Na. 1: Mahali Ambapo Furaha ya Kweli Yaweza Kupatikana (w97-SW 3/15 kur. 23)
Na. 2: Hesabu 9:1-14
Na. 3: Furahieni Wajukuu Wenu na Fanyeni Marekebisho Kadiri Mzeekavyo (fy-SW kur. 168-70 maf. 14-19)
Na. 4: Samueli (Samuel)—Kichwa: Tumikia Yehova Tangu Ujana Wako na Kuendelea
Oktoba 25 Usomaji wa Biblia: Hesabu 10-12
Wimbo Na. 125 [*Isaya 42-49]
Na. 1: Yehova Hujali Wenye Taabu (w97-SW 4/15 kur. 4-7)
Na. 2: Hesabu 10:11-13, 29-36
Na. 3: Kukabiliana na Hali ya Kupoteza Mwenzi (fy-SW kur. 170-2 maf. 20-5)
Na. 4: Safira (Sapphira)—Kichwa: Usishiriki Katika Uongo
Novemba 1 Usomaji wa Biblia: Hesabu 13-15
Wimbo Na. 64 [*Isaya 50-58]
Na. 1: Sababu Inayofanya Miujiza Peke Yake Isijenge Imani (w97-SW 3/15 kur. 4-7)
Na. 2: Hesabu 14:13-25
Na. 3: Sara—Kichwa: Urembo wa Mke Anayemhofu Mungu
Na. 4: Njia za Kikristo za Kuwaheshimu Wazazi Wazee-Wazee (fy-SW kur. 173-5 maf. 1-5)
Novemba 8 Usomaji wa Biblia: Hesabu 16-19
Wimbo Na. 78 [*Isaya 59-66]
Na. 1: Sababu kwa Nini Umaskini Haumpi Mtu Haki ya Kuiba no ref. (g97-SW 11/8 kur. 18-19)
Na. 2: Hesabu 18:1-14
Na. 3: Uwe Mwenye Upendo na Hisia-Mwenzi (fy-SW kur. 175-8 maf. 6-14)
Na. 4: Sauli (Saül) (Na. 1)—Kichwa: Uwezo Wenye Kuharibu wa Wivu na Kiburi
Novemba 15 Usomaji wa Biblia: Hesabu 20-22
Wimbo Na. 46 [*Yeremia 1-6]
Na. 1: Jinsi Biblia Ilivyotufikia—Sehemu ya Kwanza (w97-SW 8/15 kur. 8-11)
Na. 2: Hesabu 20:14-26
Na. 3: Mtazamie Yehova Sikuzote ili Upate Nguvu (fy-SW kur. 179-82 maf. 15-21)
Na. 4: Saniharibu (Sénnachérib)—Kichwa: Yehova Huokoa Watu Wake
Novemba 22 Usomaji wa Biblia: Hesabu 23-26
Wimbo Na. 59 [*Yeremia 7-13]
Na. 1: Jinsi Biblia Ilivyotufikia—Sehemu ya Pili (w97-SW 9/15 kur. 25-9)
Na. 2: Hesabu 23:1-12
Na. 3: Kuza Ujitoaji-Kimungu na Kujidhibiti (fy-SW kur. 183-4 maf. 1-5)
Na. 4: Shadraki (Shadrak)—Kichwa: Baki Bila Doa Katika Ulimwengu Usiomhofu Mungu
Novemba 29 Usomaji wa Biblia: Hesabu 27-30
Wimbo Na. 180 [*Yeremia 14-21]
Na. 1: Jinsi Biblia Ilivyotufikia—Sehemu ya Tatu (w97-SW 10/15 kur. 8-12)
Na. 2: Hesabu 27:1-11
Na. 3: Maoni Yafaayo juu ya Ukichwa (fy-SW kur. 185-6 maf. 6-9)
Na. 4: Seba (Schéba) (Na. 1)—Kichwa: Wachochezi wa Maovu Huvuna Walichopanda
Desemba 6 Usomaji wa Biblia: Hesabu 31-32
Wimbo Na. 170 [*Yeremia 22-28]
Na. 1: Mizizi ya Krismasi ya Kisasa (w97-SW 12/15 kur. 4-7)
Na. 2: Hesabu 31:13-24
Na. 3: Fungu Muhimu la Upendo Katika Familia (fy-SW kur. 186-7 maf. 10-12)
Na. 4: Sekemu (Sichem) (Na. 1)—Kichwa: Matokeo ya Ukosefu wa Adili Katika Ngono Yaweza Kuwa Yenye Kuharibu
Desemba 13 Usomaji wa Biblia: Hesabu 33-36
Wimbo Na. 51 [*Yeremia 29-34]
Na. 1: Hesabu—Kwa Nini Ni Chenye Mafaa (si-SW uku. 35 maf. 32-8)
Na. 2: Hesabu 36:1-13
Na. 3: Simei (Shiméï)—Kichwa: Utii Waweza Kuokoa Uhai Wako
Na. 4: Kufanya Mapenzi ya Mungu Mkiwa Familia (fy-SW kur. 188-9 maf. 13-15)
Desemba 20 Usomaji wa Biblia: Kumbukumbu 1-3
Wimbo Na. 159 [*Yeremia 35-41]
Na. 1: Kumbukumbu la Torati: Utangulizi (si-SW kur. 36-7 maf. 1-9)
Na. 2: Kumbukumbu 2:1-15
Na. 3: Simeoni (Siméon) (Na. 1)—Kichwa: Hasira Isiyozuizwa Hutokeza Aibu na Huzuni
Na. 4: Familia na Wakati Wako Ujao (fy-SW kur. 190-1 maf. 16-18)
Desemba 27 Kujikumbusha kwa Kuandika. Malizeni Walawi 16–Kumbukumbu 3
Wimbo Na. 192 [*Yeremia 42-48]