Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 17
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Mathayo—Yaliyomo

      • Yesu ageuka sura (1-13)

      • Imani kama mbegu ya haradali (14-21)

      • Kifo cha Yesu chatabiriwa tena (22, 23)

      • Walipa kodi kwa sarafu iliyotolewa kinywani mwa samaki (24-27)

Mathayo 17:1

Marejeo

  • +Mk 9:2-8; Lu 9:28-36

Mathayo 17:2

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “yakawa meupe.”

Marejeo

  • +Ufu 1:13, 16

Mathayo 17:5

Marejeo

  • +Zb 2:7; Isa 42:1; Mt 3:17; 2Pe 1:17, 18
  • +Kum 18:15; Mk 9:7; Lu 9:35; Mdo 3:22, 23; Ebr 2:3

Mathayo 17:9

Marejeo

  • +Mt 16:20; Mk 9:9

Mathayo 17:10

Marejeo

  • +Mk 9:11

Mathayo 17:11

Marejeo

  • +Isa 40:3; Mal 4:5, 6; Mt 11:13, 14; Mk 9:12; Lu 1:17

Mathayo 17:12

Marejeo

  • +Mk 9:13
  • +Mt 16:21; Lu 23:24, 25

Mathayo 17:14

Marejeo

  • +Lu 9:37

Mathayo 17:15

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “mwonyeshe rehema.”

Marejeo

  • +Mk 9:17-29; Lu 9:38-42

Mathayo 17:17

Marejeo

  • +Kum 32:5, 20

Mathayo 17:18

Marejeo

  • +Mt 8:13; 9:22; 15:28; Yoh 4:51, 52

Mathayo 17:20

Marejeo

  • +Mt 21:21; Mk 11:23; Lu 17:6

Mathayo 17:21

Maelezo ya Chini

  • *

    Angalia Nyongeza A3.

Mathayo 17:22

Marejeo

  • +Mt 20:18; Lu 9:44, 45

Mathayo 17:23

Marejeo

  • +Mt 16:21; Mk 9:31

Mathayo 17:24

Maelezo ya Chini

  • *

    Angalia Nyongeza B14.

Marejeo

  • +Kut 30:13, 14

Mathayo 17:25

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “kodi ya kichwa.”

Mathayo 17:27

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “sarafu ya stateri,” inadhaniwa kuwa ndiyo tetradrakma. Angalia Nyongeza B14.

Marejeo

  • +1Ko 10:32; 2Ko 6:3

Jumla

Mt. 17:1Mk 9:2-8; Lu 9:28-36
Mt. 17:2Ufu 1:13, 16
Mt. 17:5Zb 2:7; Isa 42:1; Mt 3:17; 2Pe 1:17, 18
Mt. 17:5Kum 18:15; Mk 9:7; Lu 9:35; Mdo 3:22, 23; Ebr 2:3
Mt. 17:9Mt 16:20; Mk 9:9
Mt. 17:10Mk 9:11
Mt. 17:11Isa 40:3; Mal 4:5, 6; Mt 11:13, 14; Mk 9:12; Lu 1:17
Mt. 17:12Mk 9:13
Mt. 17:12Mt 16:21; Lu 23:24, 25
Mt. 17:14Lu 9:37
Mt. 17:15Mk 9:17-29; Lu 9:38-42
Mt. 17:17Kum 32:5, 20
Mt. 17:18Mt 8:13; 9:22; 15:28; Yoh 4:51, 52
Mt. 17:20Mt 21:21; Mk 11:23; Lu 17:6
Mt. 17:22Mt 20:18; Lu 9:44, 45
Mt. 17:23Mt 16:21; Mk 9:31
Mt. 17:24Kut 30:13, 14
Mt. 17:271Ko 10:32; 2Ko 6:3
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
  • 27
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Mathayo 17:1-27

Kulingana na Mathayo

17 Siku sita baadaye, Yesu alienda pamoja na Petro, Yakobo na Yohana ndugu yake kwenye mlima mrefu wakiwa peke yao.+ 2 Sura yake ikageuka mbele yao; uso wake ukang’aa kama jua, na mavazi yake ya nje yakang’aa* kama nuru.+ 3 Tazama! wakaona Musa na Eliya wakizungumza na Yesu. 4 Ndipo Petro akamwambia Yesu: “Bwana, ni vizuri sisi tuwe hapa. Ukitaka, nitasimamisha mahema matatu hapa, moja lako, moja la Musa, na moja la Eliya.” 5 Alipokuwa bado akizungumza, tazama! wingu jangavu likawafunika, na tazama! sauti kutoka katika lile wingu ikasema: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa, ambaye nimemkubali.+ Msikilizeni.”+ 6 Wanafunzi waliposikia hilo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana. 7 Ndipo Yesu akawakaribia, akawagusa na kuwaambia: “Simameni. Msiogope.” 8 Walipotazama juu, hawakumwona mtu yeyote ila Yesu tu. 9 Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Yesu akawaamuru: “Msimwambie mtu yeyote maono hayo mpaka Mwana wa binadamu atakapofufuliwa kutoka kwa wafu.”+

10 Hata hivyo, wanafunzi wakamuuliza: “Kwa nini basi waandishi husema kwamba lazima Eliya aje kwanza?”+ 11 Akawajibu: “Kwa kweli Eliya anakuja naye atarudisha mambo yote.+ 12 Hata hivyo, ninawaambia kwamba tayari Eliya amekuja lakini hawakumtambua bali walimtendea kama walivyotaka.+ Vivyo hivyo, Mwana wa binadamu atateseka mikononi mwao.”+ 13 Ndipo wanafunzi wakatambua kwamba alikuwa akiwaeleza kumhusu Yohana Mbatizaji.

14 Walipofika karibu na umati,+ mtu fulani akamkaribia Yesu, akapiga magoti, na kusema: 15 “Bwana, mhurumie* mwanangu, kwa sababu ana kifafa na ni mgonjwa sana. Yeye huanguka ndani ya moto na ndani ya maji mara nyingi.+ 16 Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini walishindwa kumponya.” 17 Yesu akajibu: “Enyi kizazi kisicho na imani na kilichopotoka,+ nitaendelea kuwa pamoja nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni hapa.” 18 Kisha Yesu akamkemea yule roho mwovu, naye akamtoka, na yule mvulana akapona kuanzia saa hiyo.+ 19 Ndipo wanafunzi wakamjia Yesu faraghani na kumuuliza: “Kwa nini tulishindwa kumfukuza?” 20 Akawaambia: “Ni kwa sababu ya imani yenu ndogo. Kwa kweli ninawaambia, mkiwa na imani inayolingana na mbegu ya haradali, mtauambia mlima huu, ‘Ondoka hapa uende pale,’ nao utaondoka, na hakuna jambo litakalowashinda.”+ 21* ——

22 Walipokuwa wamekusanyika huko Galilaya, Yesu akawaambia: “Mwana wa binadamu atasalitiwa mikononi mwa watu,+ 23 nao watamuua, na siku ya tatu atafufuliwa.”+ Kwa hiyo wakahuzunika sana.

24 Baada ya kufika Kapernaumu watu wanaokusanya kodi ya drakma* mbili wakaja na kumuuliza Petro: “Je, mwalimu wenu hulipa kodi ya drakma mbili?”+ 25 Akajibu: “Ndiyo.” Hata hivyo, mara tu alipoingia ndani ya nyumba Yesu akamuuliza: “Unaonaje Simoni? Wafalme wa dunia hupokea ushuru au kodi* kutoka kwa nani? Kutoka kwa wana wao au kutoka kwa wageni?” 26 Alipojibu: “Kutoka kwa wageni,” Yesu akamwambia: “Basi, kwa kweli wana hawalipi kodi. 27 Lakini ili tusiwakwaze,+ nenda baharini utupe ndoano na uchukue samaki wa kwanza atakayetokea, na utakapofungua kinywa chake, utapata sarafu ya fedha.* Ichukue nawe uwape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.”

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki