WIMBO NA. 88
Nijulishe Njia Zako
- 1. Tumekutanika, Yehova Mungu; - Mwaliko wako twakubali. - Na Neno lako latuangazia, - Njia zako tunafundishwa. - (KORASI) - Nifundishe njia zako wewe; - Nieleweshe hekima yako. - Unitembeze katika kweli. - Nami nipende sheria yako. 
- 2. Hekima yako haina kifani; - Hukumu zako ni za haki. - Neno lako ni la ajabu sana. - Maneno yako yanadumu. - (KORASI) - Nifundishe njia zako wewe; - Nieleweshe hekima yako. - Unitembeze katika kweli. - Nami nipende sheria yako.